Na,Hawa Abdallah. Zanzibar.
MRAJISI wa Vyama vya Michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza amesemamabadiliko yaliyofanyika ndani ya ZFA kutoka chama hadi shirikisho yana nia ya kuhakikisha kwamba soka la Zanzibar linakuwa na linasimamiwa kwa misingi ya kimataifa.
Hayo aliyaeleza mbele ya waandishi wa habari Kuhusu muktaza mzima wa mabadiliko ya katiba ya ZFA na ambayo ilikuwaki yanaendeshwa kwa ajiliya kusimama mpira hapa Zanzibar na kuwa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF ambalo itakuwa na nia na misingi ya kuweza kusimamia soka laZanzibar.
Alisema tayari katiba hiyo imesharasimishwa na ofisi ya Mrajisi ili iweze kutumika na kwamba maeneo ambayo yamebadilika ni kama ambavyo waliona ni suala zima la chama chenyewe.
“Na naomba mufahamu kwamba mabadiliko haya yaliyofanyika inaonekana kwamba yalikuwa na nia ya kuhakikisha kwamba soka la Zanzibar linakuwa na linasimamiwa kwa misingi ambayo mashirikisho ya kimataifayanaelekeza”, alisema.
Akifafanua baadhi ya vifungu ambavyo vimebadilishwa katika katiba hiyo alisema kuwa katiba iliyopita ilikuwa inatambuwa uongozi wake kwa kuwa na rais na makamo wawili ambao walikuwa wanaongoza hii ZFA lakini kwenye mabadiliko haya suala hilo limeachwa na kilichofanywa ni Shirikisho ambalo litakuwa na makamo mmoja ambae yeye ndie atakaemsaidia rais katika kutekeleza shughuli zake.
Hivyo alisema kuwa ukiangalia maeneo hayao kile kipengele ambacho kinasomeka kwamba kutakuwa na makamo wawili mmoja Pemba na mmoja Unguja kimeondolewa na badala yake rais na makamo wake watashirikiana na kusimamia shirikisho hilo kwa pamoja.
Aidha alisema kuwa Katiba ya nyuma ilikuwa inatambuwa uwepo wa kamati tendaji isiyopunguwa watu 31 ambapo kwa upande wa Unguja walikuwa 17 na Pemba 14 kitu ambacho kilionekana kilikuwa kinakwaza kunako maamuzi kwa maana ya kwamba upande wa Unguja au Pemba kamati ilikuwa nafursa au uwezo wa kutoa maamuzi ya jambo lolote linalokuwa linahusumaendeleo au linahusu mchakato wa mazingira yoyote ya kusimamia sokala Zanzibar kitu ambacho kwa njia moja au nyengine kilikuwa kinalalamikiwa sana
“Nikiwa shahidi wa hilo kama mrajisi nilipata malalamiko mengi ambayo yalikuwa yanatolewa maamuzi, mambo mengi yalikuwa yanakwaza upande mwengine lakini kwa kweli katiba ilikuwa inaamrisha hilo na ilikuwa nishida kuyatatua mambo hayo”, alisema.
Hivyo alisema kuwa Shirikisho hilo au mabadiliko haya ambayo yamekujasasa hivi inaonekana kwamba kipengele kile kimetoka na badala yake kwamba kamati tendaji ya ZFF ambayo ndio itakayokuwa kamati tekelezaji itakuwa ipo moja ambayo ndio itakayokuwa inasimamia soka Zanzibar nzima
Kuhusu nafasi mbili za uteuzi wa rais katika katiba alisema kuwa ,Katiba iliyopita rais alikuwa na uwezo wa kuchaguwa wajumbe wawili kuwaingiza katika kamati tendaji kipengele hichi kimehusishwa lakini kimemtaka rais baada ya kuchaguwa wajumbe hao wawili ni kuweza kuwachaguwa watu ambao wanaonekana wanaweza kusaidia kutekeleza shughuli hizi za michezo na pia azingatie na maoni ya kamati tekelezaji.
Hata hivyo aliwataka waandishi pamoja na wadau kufika katika ofisi za ZFF kwa ajili ya kuweza kutafuta katiba hiyo ili kuondokana na malalamiko juu ya utekelezaji wa shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment