Habari za Punde

Timu ya Polisi Zanzibar Yajipanga Upya Kushiriki Ligi Kuu ya Zanzibar Msimu Ujao

Na Hawa Ally. ZANZIBAR
KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Nassor Salum amesema kufanya vibaya kwa timu hiyo katika msimu uliopita umetokana na kuwepo na mapungufu katika safu ya ushambuliaji.
Akizungumza na Zanzinews kocha huyo alisema  kuna nafasi nyingi katika timu hiyo ilikuwa imepwaya hususani hiyo ya washambuliaji pamoja na vioungo wa kati na mabeki wa kulia pamoja na  kushoto.
Alisema licha ya mapungufu hayo lakini timu hiyo ilijitahidi kupambana na kuhakikisha haikushuka daraja licha ya mara kwa mara kutopata matokeo mazuri hususani wanaposhuka katika viwanja vya hapa kisiwani Unguja.
“Tulianza vibaya, na mzunguko wa pili tulijitahidi kupambana hadi tukafanikiwa kuinusuru timu kutoshuka daraja, licha ya mapungu ambayo yapo katika timu lakini wachezaji waliweza kujituma kwa kiasi kikubwa.”Alisema.
Aidha alisema kuwa timu hiyo inahitaji kufanyan usajili mzuri utakaoiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika ligi ya Zanzibar ambayo vilabu vingi vinavyoshiriki ligi hiyo inawachezaji wazuri na wenye ushindani wa kweli
 Ambapo alisema  kama mwalimu yeye tayari ameshapeleka ombi juu ya idadi na nafasi anazotaka kuzisajili ikiwemo  washambuliaji 2, kiungo mmoja, beki wa kulia na wakushoto pamoja na mlinzi mmoja.
Timu ya Polisi ambayo ilimaliza ligi msimu uliopita ikiwa nafasi 9,  na point 46 huku katika michezo yake yote 35 ilipoteza michezo 10 na kutoka sare michezo 13

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.