Habari za Punde

SMZ Itaendelea Kuhishimu na Kukuza Uhuru wa Vyombo Vya Habari Zanzibar.

Na .Ali Issa Maelezo Zanzibar 3/5/2019
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Wapili wa Rais Zanzibar Mihayo Juma Nhunga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuheshimu na kukuza uhuru wa vyombo vya habari Zanzibar na uhuru wa kujieleza kama ilivyo eleza katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.
Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar katika Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya   habari duniani.
Amesema hapo kabla Serikali ya Zanzibar ilikuwa haishirikiani na wadau katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya  habari duniani, lakini sasa ni Miaka miwili Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inashirikiana na wadau wa habari.
Pia Serikali kwa sasa inafahamu,inaheshimu na itaendlea kuheshimu  uhuru huo,kwani katiba ya zanzbar imeeleza wazi na ufasaha uhuru wa kujieleza.
Aidha waziri huyo alisema pamoja na katiba ya zanzbar kutoa haki ya  uhuru wa vyombo vya  habari ,waandishi wa wahabari nao wanawajibu mkubwa kuheshimu haki na uhuru wa wengine na maslahi ya nchi.
“Msitumie kalamu zenu kuwatesa wengine kwa kutumia TV,Radio na Magazeti namitandao, tufanye kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya kazi yetu,alisema Naibu Waziri huyo.
Hata hivyo Waziri aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuna uhuru usio na mipaka,hivyo wawe waangalifu juu ya kile wanacho kiandika lazima wapate vibali na ruhusa kwa kufanya uchambuzi wa taarifa anayo itoa.
“Tujiulize ni wangapi tumewakosea tumewaandika vibaya kwa chuki au sababu nyengine yoyote ile ambao wangetamani kwenda mahakmani lakini wanachelea taratibu za kimahakama huchukuwa mda na  watapoteza kupata hakizao,”aliongeza kusema.
Wazri huyo aliwambia Wandishi wa Habari wawe na utamaduni wa kuombaradhi wanapomkosea mtu au kuzusha jambo na waangalie huko usoni kuwa Tanzania itakuwa na uchaguzi mkuu wa kitaifa wa viongozi mbali mbali  hivyo wasikubali kutumiwa kuichafua nchi.
Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari na Mambo ya Kale DtK.Salehe Yussuf Mnemo  alisema kua mpaka sasa hakuna kumbukumbu ya  lalamiko lolote linalo ikosoa Serikali kuwa Zanzibar haina uhuru wa vyombo vya habari, bali machapisho yote yalioandikwa iliisifu  inaheshimu Uhuru wa vyombo vya habari Nchini.
Aidha katibu huyo aliwahakikishia waandishi wa habari kuwa changamoto zilizotajwa zitatatuliwa ili kuweza kufanya kazi kwa kujiamini zaidi.
Nae Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar DKT. Juma Muhamed Salum alisema kuwa dhana ya habari katika uchaguzi na demokrasia inakusudia dhima na dhamana ilio pewa vyombo vya Habari katika kudumisha demokrasia.ni sehemu moja muhimu ya kuwa na maendeleo.
Alisema dhana hiyo inaungana na masuala ya uhuru wa vyombo vya habari katika kutoa habari zenye maendeleo endelevu na kuitanabaisha jamii kwa kuikosoa ili kuleta maendeleo.
Aidha aliwataka wandishi kujitathmini wapi wanatoka na wapi wanakwenda,kuangalia mafanikio na kasoro ili kuleta weledi katika sekta hiyo.
Mkurugenzi huyo alieleza changamoto zinazo ikumba sekta hiyo ni pamoja na kutokuwepo Sheria mahususi ya Habari,kutokuwepo vyama maalumu vya wafanyakazi wandishi wa habari katika kuleta maslahi yao.
Pia kuwepo malipo duni yasio zingatia Sheria za Serikali kwa baadhi ya vyombo vya habari kwa wandishi wake na ukosefu wa uhuru wa uhariri.
Siku ya uhuru wa habari duniani huadhumishwa kila ifikapo mei tatu na ujumbe wa mwaka huu ni wajibu wa vyombo vya Habari katika uchaguzi na demokrasia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.