Habari za Punde

Wajasiriamali Wanawake Watakiwa Kuepuka Tabia ya Utegemezi.

Wajasiriamali kutoka maeneo mbali mbali wakipatiwa mafunzo ya ujasiri Mali yalioendeshwa na watendaji kutoka idara ya mikopo kupitia Wizara ya Kazi, uwezeshaji, wazee wanawake na watoto hapo Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.
 Msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzinar anayeshughulikia Ustawi wa Jamii Bibi Siti Abasi Alia kitoa Mada kwenye Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo Bw. Suleiman Haji akiwashauri wajasiriamali wanaopatiwa mafunzo kujitokeza kujaza fomu za maombi ili muda utakapofika Serikali iweze kuwapatia mitaji.
Baadhi ya Wajasiriamali kutoka maeneo mbali mbali wakiwa makini kufuatilia Mada tofauti zilizowasilishwa kwao wakati wa kujengewa uwezo wa kujiendesha Kimiradi wakati wanapopatiwa Mitaji.
Picha na – OMPR – ZNZ.



Na.Rashida Abdi.OMPR. 
Msaidizi wa Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzinar anayeshughulikia Ustawi wa Jamii Bibi Siti Abasi Ali amewaomba wajasiriamali wanawake kuepuka  tabia ya utegemezi kwa kuanzisha miradi midogo midogo itakayowasaidia kuwaingizia kipato kwa lengo la kujikomboa na umaskini.
Alisema kuna kila sababu kwa wanawake kuanzisha na kuendeleza miradi kwa kufungua biashara ndogo ndogo zitakazowaingizia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku ili kuepuka kuwategemea wanaume katika kuendesha familia
Bibi Siti ameleza hayo katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais uliopo Vuga kupitia kikao maalum cha kuwapatia mafunzo wajasiriamali kutoka maeneo mbali mbali yalioendeshwa na watendaji kutoka idara ya mikopo kupitia Wizara ya Kazi, uwezeshaji, wazee wanawake na watoto.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mkurugenzi kutoka Idara ya Mikopo Bw. Suleiman Haji aliwashauri wajasiriamali hao kujitokeza kwa wingi katika kujaza fomu za maombi ili muda utakapofika Serikali iweze kuwapatia mitaji.
Alisema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa wajasiriamali wa Zanzibar kutochangamkia fursa hiyo na kukosa uthubutu badala yake kupelekea kuwanufaisha watu wengine kutoka mbali hali inayopelekea wajasiriamali hususani wanawake kuishi katika maisha duni yenye utegemezi ndani yake.
Pamoja na Mambo mengine Nd. Suleiman alisema changamoto nyengine wanayokumbana nayo katika mazingira yao ya kazi ni upotoshaji wa kutoa taarifa kutoka kwa wajasiriamali wanapofika Afisini kwao kwa ajili ya kuomba mikopo sambamba na tatizo la urejeshaji wa mikopo hiyo.
Mkurugenzi Suleiman alitoa wito kwa watu ambao wamenufaika na mkopo huo kujitahidi kurejesha mikopo walioyochukuwa ndani ya wakati ili iweze kuwanufaisha na watu   wengine wanaohitaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.