Habari za Punde

Wananchi Washiriki katika Mazishi ya Mwanasiasa Mgongwe Zanzibar Marehemu Ramadhan Abdalla Shaban Yaliofanyika Kijiji Kwao Uzini Wilaya Kati Unguja.t

Marehemu Ramadhani Abdalla Shabani Azikwa leo Kijiji Kwao Uzini Mkoa wa Kusini  Unguja Wilaya ya Kati 
Umati wa Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Mwana siasa Mkongwe  Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji kwake Uzini.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakimuombea Dua Marehemu Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban aliyefariki katika Hospitali ya Aga Khan Mjini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakilichukuwa janaezea la Marehemu Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban kuelekea katika makaazi yake ya Kudumu {Kaburini}.
Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananhi pamoja na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakiendelea na harakati za kuufukia mwili wa Marehemu Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban hapo Kijijini kwao Uzini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia mchanga ndani ya Kaburi la Marehemu Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban hapo Kijijini kwao Uzini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohgamed Aboud Mohamed akitia mchanga ndani ya Kaburi la Marehemu Maalim Ramadhan Abdullah Shaaban hapo Kijijini kwao Uzini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.