Habari za Punde

Waombelezaji na Wananchi Wafika Nyumbani Kwa Dk. Mengi Jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria wa familia,Michael Ngalu  akizungumz na waandishi wa habari ambapo amesema  kwa sasa maandalizi yanaendelea na kwamba taarifa za msiba zitatolewa kesho mchana.

Waombolezaji wamesema Mwenyekiti wa makampuni ya IPP marehemu Dkt. Reginald Mengi atakumbukwa na Watanzania wote kwa jinsi alivyojitoa maisha yake kwa ajili ya maisha ya wengine, hasa wanyonge na wenye mahitaji maalumu.

Wamesema hayo walipomiminika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es salaam kutoa pole na rambirambi kwa wafiwa. Dkt. Mengi alifariki dunia mapema asubuhi ya  Alhamisi akiwa Dubai kwenye matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema  wakati alipofika nyumbani hapo kwamba msiba wa Mengi ni mkubwa na umeligusa Taifa kutokana kwa  kujitoa kwake katika kuisaidia jamii. 

"Mzee Mengi alikubali kujitoa kwa watu maskini kwenye jamii ambapo aliahidi kuwajengea uwezo walemavu ili kuondokana na umaskini" amesema Makonda. "Matamanio yangu mazishi ya Mzee mengi watu wajitokeze kwa wingi ili kumuenzi mzee wetu huyu." 
Mkuu huyo wa mkoa amesema baada ya ratiba ya mazishi kufahamika kutoka kwa wanafamilia angependa watu wajitokeze kwa wingi kumpa marehemu upendo na heshima anayostahili. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe amesema kifo cha Dkt. Mengi ni pigo kwa taifa na itakuwa vigimu kumpata mtu kama huyo kirahisi.

Akizungumza nyumbani hapo, Mhe.  Mbowe amesema ndugu wa karibu wa familia ndio wanaanza kufika hivyo taratibu nzima kuhusiana na msiba huu zitatolewa baadae"
Mhe Mbowe amesema Marehemu Mzee Mengi alikuwa mtu wa watu wote na kwamba alijali sana walemavu, wanamichezo pamoja na tasnia nzima ya mambo ya habari. 

"Kwa niaba ya wanachi wa Moshi,wanachama wa vyama vyote hasa wanachama wa wa chadema pamoja na watanzania wote nitoe pole kwa walioguswa na msiba huu.

"Niwaambie tu itachukua miaka muda mrefu kuziba pengo aliloacha Mzee Mengi kwani alikuwa mdau wa uwekezaji aliyejali wanyonge na kuondoka kwake ni pigo kubwa kwa Taifa"amesema.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda  akiwasili kwenye Msiba wa Mwenyekiti wa kampuni za IPP Regnaldi Mengi nyumbani kwa marehemu Kinondoni  jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe  akizungumza na waandishi wa habari leo alipofika kufariji wafiwa nyumbani kwa Dkt  Regnaldi Mengi Kinondoni  kufwatia kifo cha Mwenyekiti huyo aliefariki usiku wakuamkia Mei 2,2019 dubai.
Mwanasheria wa familia,Michael Ngalu  akizungumz na waandishi wa habari ambapo amesema  kwa sasa maandalizi yanaendelea na kwamba taarifa za msiba zitatolewa kesho mchana.
 Waombolezaji wakiwa nymbani kwa  Dkt  Regnaldi Mengi Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakiwa katika majukumu yao nyumbani kwa Dkt  Regnaldi Mengi  Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.