Habari za Punde

Jukwaa la Walimu Wazalendo Kinondoni Wachangia Damu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma

Naibu Katibu Mkuu wa Jukwa la Walimu Wazalendo Taifa, Mwl. Mkomanile Mahundi akichukulia kipimo cha damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu katika Kituo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma leo. Wajumbe wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania toka wilaya ya Kinondoni wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kufanya shughuliza kijamii ikiwemo usafi na kuchangia damu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu Tano katika kutoa huduma bora za Afya nchini.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania toka wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akichangia damu katika Kituo cha Damu salama mkoa wa Dodoma walipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma leo na kufanya shughuli za kijamii ikiwemo usafi na kuchangia damu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu Tano katika kutoa huduma bora za Afya nchini. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam, Ambwene Kajula.
Naibu Katibu Mkuu wa Jukwa la Walimu Wazalendo Taifa, Mwl. Mkomanile Mahundi (kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Walimu Wazalendo wilaya ya Kinondoni wakichangia damu katika Kituo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma leo. Wajumbe wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania toka wilaya ya Kinondoni wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kufanya shughuliza kijamii ikiwemo usafi na kuchangia damu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu Tano katika kutoa huduma bora za Afya nchini.
Baadhi ya wajumbe wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania toka Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakipima uzito wakati wa zoezi la uchangiaji damu katika Kituo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma leo. Wajumbe wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania toka wilaya ya Kinondoni wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kufanya shughuliza kijamii ikiwemo usafi na kuchangia damu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu Tano katika kutoa huduma bora za Afya nchini.
Msimamizi Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Dodoma, Dkt. Leah Kitundwa akitoa maelezo kuhusu uchangiaji wa damu kwa wajumbe wa Jukwa la Walimu Wazalendo Tanzania toka Wilaya ya Kindondoni Dar es Salaam walipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kufanya shughuliza usafi pamoja na kuchangia damu katika kituo hicho leo jijini Dodoma kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu Tano katika kutoa huduma bora za Afya nchini.  Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Wilaya ya Kinondoni Mwl. Leah Mkinga.
(Picha na Frank Shija – MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.