Habari za Punde

Ufungaji wa Bonaza la Michezo la Kupiga Vita Utumiaji wa Dawa za Kulevya

Na.Mwanajuma Juma.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayuob Mohammed Mahmoud amesema kuwa kila mmoja anawajibika kuhakikisha vijana wao wanaondokana na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Ayuob aliyaeleza hayo katika hafla ya ufungaji wa Bonanza la Michezo la mpira wa miguu lililowashirikisha timu za madaraja ya vijana ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya siku ya kupinga vitendo vya utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Alisema kuwa vita dhidi ya dawa za kulevya sio vidogo kutokana na kuwa na mtandao mpana lakini hali hiyo haimaanishi watu kurudi nyuma katika kupingana navyo.
‘Sote tunawajibu wa kupiga vita juu ya suala hili, na kila ambae anahisi ana mdogo wake au mwanawe anautumia madawa haya awe yupo tayari kumtibu na kumlinda ili aweze kuacha”, alisema.
Alifahamisha kwamba vijana wanapojiingiza katika madawa ya kulevya wanapoteza nguvu kazi ya taifa na kushindwa kufikia malengo yake ya kuwa na maendeleo endelevu.
“Vita hivi si ndogo lakini tusirudi nyuma, songa mbele, pigana na pambana, kwani nguvu kazi ambayo tunaipoteza inayotukosesha kufikia mafanikio”, alisema.
Mapema akisoma risala Mjumbe kutoka Taasisi ya Corner Stone Recovering inayojishughulisha na vijana walioacha utumiaji wa madawa hayo ya kulevya Nassor Muhsin Ali alisema kuwa wameamuwa kutumia michezo kupiga vita dhidi ya suala hilo kwa kuamini kuwa nayo ni miongoni mwa njia muhimu ya kuweza kufikisha ujumbe kwa vijana.
Alisema kuwa taasisi yao  imekuwa mdau mkubwa wa vita dhidi ya madawa ya kulevva kwa kupitia program ya Sporst not drug okoa vijana ambayo inalenga kutumia michezo ili kuweza kushajiisha vijana waliofanya maamuzi ya kuacha kujikita katika michezo na kuibuwa vipaji vyao ikiwa ni mpira wa miguuna kuweza kutengeneza ajira kwa vijana hao.
Alieleza kuwa mbali na ambao wamejiingiza lakini pia program hiyo huwatumia vijana ambao wapo katika hatarishi na wao kujikita katika michezo kwa kutengeneza vipaji vyao na wao kutengeneza ajira.
Bonanza hilo limeandaliwa na taasisi hiyo ya Corner Stone Recovering kwa kushirikiana na taaisis ya Mimi na wewe Foundation lilishirikisha vilabu nane vya madaraja ya vijana ambapo timu ya soka ya vijana ya Mlandege ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Blacksailor mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.