Habari za Punde

AGIZO LA WAZIRI JAFO LATEKELEZWA KWA VITENDO WILAYANI PANGANI


Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akiuzngumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule  za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo tatu za uzalendo ikiwemo  ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda TanzaniaDSC_0077 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akiuzngumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule  za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo  ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
IMG_9238  Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kushoto  akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange kulia wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
IMG_9237 Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani wakimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
IMG_9246 Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
IMG_9286
 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Funguni
IMG_9268
NA MWANDISHI WETU,PANGANI.
AGIZO La Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule  za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo  ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania  limeanza kutekelezwa  kwa vitendo wilayani Pangani mkoani Tanga.
Utekelezaji huo umeanza leo Julai 8 mwaka huu kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wilayani humo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kutembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji huo.
Agizo hilo la Waziri Jaffo alilitoa hivi karibuni wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Umoja wa shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) yaliyokuwa yakifanyika mkoani Mtwara ambapo aliagiza kwamba wakati wanafunzi watakapofungua shule wanatakiwa kuimba nyimbo tatu kabla ya kuingia madarasani asubuhi Nyimbo hizo ni wimbo wa Taifa,Wimbo wa Uzalendo (Tanzania tanzania) na Tazama Ramani utaona nchi nzuri kwa maafisa  elimu Kata na wakuu wa shule wasimamie hilo.
Akizungumza mara baada kikao cha wadau wa elimu kilichohusisha wakuu  wa shule za msingi na sekondari,Waratibu Elimu Kata,Watu wa tume ya Utumishi wa walimu wa kudhibiti ubora wa elimu ambacho kilikuwa ni mahususi ya kuona namna ya kuendeleza utekelezaji wa agizo hilo na baadae kutembelea kwenye shule hizo kuona namna wanafunzi  wanavyoweza kuimba  nyimbo za uzalendo wanapokuwa shuleni na hivyo kujiridhisha
Alisema kwamba wao kama wilaya wataendelea kulisimamia ipasavyo na kulitekeleza agizo hilo kwa vitendo huku wakianza na hatua ya kwanza kwa kuwaita kwenye kikao hicho huku akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje na Wakuu wa Idara kwa kuweka mikakati ya kuona namna gani agizo hilo linatekelezwa kwa kuhakikisha wanaandika upya kwenye makaratasi na kubandikwa kila darasa wanalosoma wanafunzi.
"Lakini kubwa ni kwamba kila mwanafunzi achague kwenye somo wanayosoma achukue daftari moja aandika nyimbo hizo vizuri kwa nyuma kujikumbusha mara kwa mara kwa lengo la kuweza kuutambua na kuweza kuimba kwa ufasaha zaidi kila wakati "Alisema
Hata hivyo Katibu Tawala huyo aliwaagiza Waratibu wa kata wahakikishe maelekezo yaliyotolewa yanafanyiwa kazi na kupita kwenye  kukagua kuona
 kama nyimbo hizo zimefundishwa.
Awali akizungumza Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George alisema kwamba wamefika kwenye shule hizo kutekeleza agizo la Jafoi shule zao zirudi kwenye msingi ya kukumbushia nyimbo za uzalendo kwa wanafunzi.
Alisema pia wataendelea kuwajenga vijana kuhusu uzalendo wakiwa wadogo ili kutengeneza Taifa Bora la kesho ambalo litakuwa chachu ya maendeleo kwa watanzania
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Pangani  Isaya Mbenje alisema kwamba ni imani yake kwamba watendaji wa sekta ya elimu watakwenda kufanyia kazi kwa kuweka uelewa wa pamoja.
Alisema kwamba uelewa huo unaweza kuwasaidia kuona namna ya utekelezaji wa agizo hilo la serikali katika kujenga nidhamu,uzalendo wa vijana wa shule za msingi na sekondari za serikali wilayani humo.
Hata hivyo naye pia Afisa Elimu Taaluma wa wilaya ya Pangani Marietha alisema kwamba wanamshukuru Waziri Jaffo ambaye  alihuisha uzalendo wa nchi kutokana na kwamba watu walikuwa wamejisahau sana nyimbo hizo miaka ya nyuma zilizokuwa ngao lakini kutokana na kwamba hapo katikati walipotea na kusahau hivyo wanahaidi kufanya vizuri sana

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.