Habari za Punde

Mfumko Wa Bei za Bidhaa Umepungua Kwa Asilimia 3.1 Kwa Bidhaa Tafauti Zanzibar.

Na. Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar.   4-7-2019.
MKUU Wa Kitengo cha bei Khamis Abdulrahman Msham amesema hali ya mfumo wa bei za bidhaa umepungua kutoka asilimia 3.1kwa mwaka uloishia June 2019 hadi kufikia asilimia 2.7kwa mwaka uloishia Mei 2019 kwa  bidhaa zinazotumiwa na wananchi tofauti.
Hayo ameyasema leo huko katika Ukumbi ya  Ofisi ya Mtakwimu ilioko Mazizini wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa kuripoti taarifa za bei kuhusu kushuka kwa bidhaa ikiwemo chakula.
Amesema mfumuko wa bei za bidhaa umepungua ikiwemo chakula kama vile mchele wa mapembe, mchele wa basmati, ndizi na samaki  na pia mafuta ya taa.
Pia amesema hali ya uchumi inaimarika vizuri ukilinganisha na nchi nyengine za Afrika Mashariki kwa jinsi kasi ya  kupanda imepungua kutokana na uzalishaji uliyo mzuri.
Nae Meneja wa Idara ya Uchumi Tanzania Bank of Tanzania BOT Moto Ng’winganele Lugobi amesema hali ya mfumuko wa bei kwa sasa ni mzuri kutokana na uzalishaji wa mavuno uko vizuri na kuwataka wananchi kuzalisha mavuno kwa wingi.
Kwa upande wa Mhadhiri wa Uchumi kutoka chuo kikuu cha Taifa SUZA Suleiman Msaraka Pinja amesema Serikali ikianza bajeti huweka malengo yake hivyo lengo la mfumko wa bei usizidi ili wananchi waweze kumudu  bei za bidhaa.
Hivyo lengo limetimia mfumo wa bei umeshuka na kuwataka wananchi waendelee kuzalisha chakula kwa utaalamu zaidi kwani wakifanya hivyo mfumko wa bei hautokuwa mkubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.