Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Mabodi Awaonya Wana CCM Wanaotumia Vibaya Mitandao ya Kijamii.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani huko Mbweni Unguja.
WAJUMBE wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.

Na.Is -Haka Omar .
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amewataka Viongozi wa CCM kutumia Vikao halali vya Kikatiba na Wazee wa Taasisi hiyo kutafuta ufumbuzi wa changamoto hasa tuhuma za kisiasa badala ya kutumia Mitandao ya Kijamii.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani,uliofanyika katika Ofisi ya CCM iliyopo Mbweni Unguja.
Dk.Mabodi alisema kila Mwanachama ndani ya CCM ana Haki na Wajibu wa kutumia miongozo na kanuni ya kikatiba kutafuta ufumbuzi wa changamoto yoyote inayomkabili kisiasa na sio kutumia majukwaa mengine yasiyokuwa rasmi.
Alieleza kwamba ni kosa kimaadili jambo lolote linalogusa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi kulijadili na kulitolea maamuzi kinyume na utaratibu uliowekwa na miongozo ya Chama.
Kupitia Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema kiongozi,Mtendaji na Mwanachama yeyote mwenye malalamiko juu ya mwenzake anatakiwa kufuata tararibu zilizowekwa kuanzia ngazi za Mashina hadi Taifa.
“Nakemea tabia ya baadhi ya Wanachama na Viongozi kutumia Mitandao ya Kijamii kuchafuana kisiasa sio utaratibu wa CCM, na yeyote tutakayembaini kufanya hivyo basi tutamchukulia hatua za Kimaadili kwa mujibu wa Miongozo yetu.”, alisema Dk.Mabodi.
Pamoja na hayo aliwakumbusha Wajumbe wa Mkutano huo kuwa ni marufuku kwa Mwanachama yeyote kufanya kazi ya udalali wa kisiasa wa kuwapigia kampeni za kuwania Uongozi wa ngazi yeyote baadhi ya Makada mwaka 2020 kabla ya kampeni hizo kuruhusiwa kikatiba.
Aliwapongeza Viongozi wa Wilaya hiyo kwa kufanya kikao hicho kinachowaunganisha Wanachama na Utendaji wao katika kuandaa mazingira ya Ushindi wa CCM kwa mujibu wa Ibara ya Tano ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977.
Aliwataka Wabunge,Wawakilishi na Madiwani kuendelea kutekeleza Ilani ya CCM katika maeneo yao ili Wananchi wanufaike na huduma bora za maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud, aliwataka Wanachama wa CCM kuungana pamoja katika kuandaa ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na kubadilika kitabia kwa kutofanya kazi kwa mazoea.
CAPTION
0034-NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani huko Mbweni Unguja.
0065-WAJUMBE wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dimani wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.