Habari za Punde

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde Awataka Vijana Kuenzi Mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi, Watumishi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na wakazi wa Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba akielezea jambo kwa vijana 8 walioshiriki katika shughuli hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Mwanaidi Ali.
Baadhi ya Watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwaaga vijana hao.
Sehemu ya Vijana wanaotarajiwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima huo, Julai 26, 2019.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi Bendera ya Taifa Kiongozi wa msafara huo Bw. Agustine Gusha mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (wenye kofia ya Bluu) akiwasindikiza vijana hao kuashiria kuanza kwa safari yao ya kupanda Mlima huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akiwaaga Vijana hao nane (8) kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja alipowasindikiza vijana hao waliokuwa wakipanda Mlima huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kippi Warioba.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima huo.
Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho akimfafanulia Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusi hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga vijana hao.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akielezea kuhusu vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akijadili jambo na Kamishna Mwandamizi wa Kanda ya Kaskazini, Herman Batiho alipowasili katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuwa kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa awamu ya pili.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghirwa alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na vijana watakaopanda Mlima Kilimanjaro, alipowasilia Mkoani huo kwa lengo la kuwaaga vijana hao.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Na; Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amewataka vijana kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa wazalendo na wenye mshikamano katika kujenga Taifa.
Mhe. Mavunde amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga vijana kutoka Mkoa wa Songwe, Arusha, Tanga, Kaskazini Unguja na Kusini Unguja kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kuiga kivitendo yale yote yaliyotendwa na waasisi wa taifa hili, Mwl. Julius K. Nyerere na Hayati Mzee Abeid Karume kwa kuendelea kudumisha upendo, amani na mshikamo kwa mustakabali wa Taifa.
“Vijana waliowengi kipindi hiki wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda taifa lao hali ambayo inatubidi tujitahmini na kuenzi falsafa walizokuwa nazo waasisi wetu ambao waliweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote,” alisema Mavunde
Akitolea mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza masuala mbalimbali ya kitaifa wakati wote ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana waliopanda mlima huo awamu ya kwanza na awamu hii ya pili kwa kuonesha ushujaa na uzalendo kwa Taifa lao ikiwemo kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza sekta ya utalii.
Aidha, Naibu Waziri Mavunde alitoa wito kwa vijana kuacha kukaa kwenye vijiwe na kujihusisha kwenye mambo yasio na tija, bali wajishughulishe kwenye miradi mbalimbali itakayo wawezesha kiuchumi na kusaidia kukua kimaendeleo, kwa kuwa waasisi wa taifa walikuwa wachapakazi, waadilifu na wabunifu ambao ni mfano mzuri wa kuigwa.
“Hakuna nchi yoyote dunia ambayo inaweza kuendelea pasipo kuhusisha nguvu kubwa ya vijana katika maendeleo ya taifa,” alieleza Mavunde
Aliongeza kuwa ili kufikia malengo kwenye uchumi wa viwanda ni lazima vijana wazingatie uzalendo, utaifa na bidii katika kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa kitendo cha vijana hao kushiriki katika kupanda Mlima huo ni jambo muhimu kwa taifa na inaashiria namna gani vijana wameanza kutambua historia ya waasisi wa taifa lao.
Naye, Kiongozi wa Vijana hao waliopanda Mlima Kilimanjaro Bw. Augustine Gusha aliunga mkono maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na alitumia nafasi hiyo kuwasihi vijana kudumisha amani ya nchi wakati wote.
Katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana inaratibu shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Vijana 100 kwa ajili ya kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Awamu ya kwanza vijana walipanda mlima huo tarehe 26 Machi, 2019 na awamu ya pili 26 Julai, 2019. Awamu ya Tatu itakuwa mwezi Oktoba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.