Habari za Punde

PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA NA WANANCHI KUFIKA KWENYE BANDA LA MFUKO HUO KUPATA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA


 Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akiwahudumia wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Juni 30, 2019.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAONESHO ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, tayari yamepamba moto ambapo Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, ametoa wito kwa Wanachama wa Mfuko huo pamoja na Wananchi kufika kwenye banda hilo ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.

Bi. Chiume amesema, banda la PSSSF liko jengo namba 13 mkabala na jengo la matangazo ndani ya viwanja vya Maonesho Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
"Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama wanahitaji kuelimishwa kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao ni watumishi wa Umma." Alifafanua Bi. Chiume.

Alisema uduma za PSSSF zitatolewa kwenye jingo moja ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Maonesho hayo yameanza Juni 28 na yatafikia kilele Julai 13, 2019 na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto), pamoja na Afisa Matekelezo wa NSSF, Bi.Diogi Janguo, (wapili kulia) na Mtaalamu wa mifumo ya computer, NSSF Bi.Grace Magigile wakati Bw. Erio alipofika kwenye jengo namba 13 ambalo Mifuko yote miwili ya PSSSF na NSSF inatoa huduma kwa ushirikiano katika jengo hilo. Itakumbukwa kuwa PSSSF ni Mfuko ulioundwa kuhudumia Watumishi wa Umma na NSSF kuhudumia Sekta binasi.
 Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto), akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda hilo.
Jengo namba 13 ambalo ndipo ilipo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF.
Timu ya PSSSF ikiongozwa na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ikiwa tayari kutoa huduma bora kwa wanachama na wananchi watakaofika kwenye banda hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.