Habari za Punde

Tamwa yaiomba Serikali kuweka mazingira sahihi ya utekelezaji wa sheria ya makosa ya jinai

Na Hawa Ally

CHAMA cha waandishi wake habari wanawake TAMWA Zanzibar kimeiomba serikali kuweka mazingira mwafaka ya utekelezaji wa sheria ya makosa ya jinai ikiwa pamoja na uwepo wa vitendea kazi stahiki katika ufatiliaji wake kesi za mokosa hayo.

Hayo yameelezwa na meneja sera na utetezi wa TAMWA Zanzibar Haula Shamte wakati akizungumza na waandishi wa Habari huko ofisi ya chama hicho Tunguu.

Alisema inakatisha tamaa kusikia polisi wakisema wanashindwa kufuatilia kesi kwa sababu ya kutokuwa na usafiri au upelelezi kutoka milika hususani kwa kesi za ubakaji na mauwaji jambo ambalo upelekea hata vitendo  vintendo vya udhalilishaji  kuendelea katika Jamii.

Alisema vitendo vya ukatili wa kijinsia visiwani hapa vinatishia amani na usalama hasa wanawake na watoto ambapo ukatili huo haushii kwenye kudhalilisha kingono bali hata katika kutoa uhai kwa wanawake wanaodhalilishwa.

Alisema TAMWA kupitia timu ya waandishi wa habari imefuatilia kesi za mauji ya wanawake na watoto yaliyotokea kuanzia mwaka 2016 hadi 2019 na kubaini kesi 13 zilizoripotiwa ni kesi tatu ambazo zinaendelea mahkamani.

Haula alisema kati ya kesi hizo Kesi tano zipo polisi,kesi moja faili lake lipo kwa mkurugenzi wa mashtaka na kesi 4  zimefutwa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Tamwa Zanzibar DK Mzuri Issa ameviomba vyombo vya maamuzi kubuni mbinu zitakazopelekea kesi za ukatili zinapatiwa hukumu kwa wakati ili kuondosha vitendo hivi ambavyo vinatia doa nchi.

Alisema polisi watumie mbinu zao ambazo zitaharakisha kukamilika kwa upepelezi wa kesi hizi za udhalilishaji na mauwaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.