Na.Mwanajuma Juma.
TIMU ya soka ya Mnazi Mkali imetangulia hatua ya robo ya fainali ya michuano ya kombe
la Kipwida kufatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kisakasaka.
Mnazi mkali inakuwa timu ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kufikisha pointi saba
katika kundi D ambalo linaloundwa na timu za Langasta, Mafriji, Sarayevo Home
Boys na Kisakasaka ambazo zote zina pointi moja moja.
Katika mchezo huo timu hiyo ambayo imebakisha mchezo mmoja mabao yake yaliwekwa
kimiyani na wafungaji wake Abdul Hamad dakika ya 78 na Hair Abuu dakika ya 82.
Michuano hiyo leo itaendelea tena kwa kupigwa mchezo wa kundi A ambao utawakutanisha
Lion Kids na Nyamanzi City.
No comments:
Post a Comment