Na. Mwanajuma Juma.
ALIEKUWA kocha wa timu ya soka ya Pamba SC Ali Omar Kisaka amesema kuwa
kwa sasa yupo na yupo tayari kufanya kazi
na timu yoyote ambayo itamuhitaji baada ya
kumaliza mkataba na timu hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
Kisaka alisema kuwa anashukuru kumaliza
mkataba na timu hiyo bado hajapokea
taarifa yoyote kutoka kwa uongozi baada ya
kumaliza ligi.
Kisaka ambae aliifundisha timu hiyo baada
aliekuwa kocha wao Juma Sumbu kupata
maradhi ya kupooza alisema kuwa anashuku
ru kumaliza ligi hiyo na kuibakisha daraja
ingawa alishindwa kuipandisha na
kucheza ligi kuu.
“Mpaka sasa nipo, nimemaliza mkataba na sijapokea taarifa yoyote kutoka kwa uongozi
wangu lakini kama kutatokea timu nipo tayari kufanya nayo kazi”, alisema.
Akizungumzia ligi ya Tanzania Bara alisema kuwa ni ngumu na yenye ushindani sambamba
na kuwepo kwa vitisho hasa timu inapotoka kwenda kucheza katika mkoa mwengine.
Hata hivyo alisema kuwa kupitia ligi hiyo ameweza kupata mafanikio makubwa ikiwemo
akili yake kukuwa kielimu zaidi.
“Nimefanya vizuri japo mtu hajioni mwenyewe aneona yupo juu lakini nimepiga hatua”,
alisema.
Timu hiyo aliichukuwa ikiwa katika nafasi ya sita pointi 14 ambapo alifanikiwa kuifikisha
hatua ya kupanda lakini
lishindikana baada ya kutolewa katika mchezo wa mwisho na timu ya Kagera Sugar na
kushindwa kupanda.
No comments:
Post a Comment