Habari za Punde

Wakala wa Ununuzi Yawatangaza Wazabubi 3332 Watakaotoa Huduma Mkoa wa Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu, Maelezo -Dar es Salaam 4.Julai, 2019
WAKALA wa Huduma ya Ununuzi Tanzania (GPSA) katika mwaka 2019/2020 imewatangaza wazabuni 3032 walioshinda zabuni kwa ajili kutoa na kusambaza huduma mbalimbali za manunuzi katika Ofisi i za Serikali ikiwemo Wizara, Idara, Wakala na Taasisi mbalimbali za umma katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza katika leo Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere, Meneja wa GPSA Kanda ya Dar es Salaam, Emmanuel Msongole alisema zabuni hiyo ilianza kutangzwa na taasisi hiyo kuanzia mwezi Januari mwaka huu.
Msongole alisema taasisi hiyo inaendelea kusimamia misingi ya kisheria katika kupata wazabuni wenye sifa na vigezo vyote vinavyotakiwa na  Serikali na kamwe haitaruhusu kuvunjwa kwa taratibu za kisheria ikiwemo utoaji wa rushwa katika zabuni kwa kuwa jambo hilo limekuwa likiathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi kwa kuagiza vifaa vilivyo chini ya kiwango.
“GSPA tumekuwa tukiimbia wimbo wa rushwa kwa kuwa ni adui wa maendeleo na mara nyingi imekuwa ikiathiri utoaji wa huduma ikiwemo ununuzi wa vifaa dhaifu na kuiletea hasara serikali” alisema Msongole.
Kwa mujibu wa Msongole alisema katika zabuni hiyo jumla ya makampuni 3100 zilioomba zabuni za usambazaji wa huduma, ambapo kampuni 68 zilishindwa kukamilisha taratibu za msingi na hivyo kukosa sifa ya kutoa huduma zake katika Ofisi za Umma.
Aidha Msongole aliongeza kuwa GPSA imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara kwa wazabuni wote ili kuweza kufahamu namna bora ya kujaza fomu za maombi ya zabuni na kuyawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa sifa za msingi wakati wa kuomba zabuni katika taasisi mbalimbali za umma na za binafsi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.