Habari za Punde

Rais ZFF avitaka vilabu kuhamasisha mashabiki wahudhurie kwa wingi viwanjani ligi itakapoanza

Na Hawa Ally, ZANZIBAR

RAIS wa shirikisho la Soka Zanzibar ZFF Seif Kombo Pandu amevitaka vilabu kuhamasisha mashabiki wao kuja uwanjani pindi ligi itakapoanza katika msimu huu wa 2019/2020 iliyopangwa kuanza August 25. 

Aliyasema hayo katika ziara yake maalum ya kuzungumza na vilabu vya vinavyoshiriki ligi Kuu ya Zanzibar na ligi daraja la Kwanza Kanda ya Unguja ambapo alisema vilabu vya Zanzibar asilimia kubwa vinakabiliwa na changamoto ya umaskini hali inayopelekea hata kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na walimu wa timu hizo. 

Alisema Ili kukabiliana na changamoto hiyo ya fedha watumie vyombo vya habari katika kuhamasisha mashabiki wa timu hizo kufika uwanjani Ili asilimia za viingilio watakazopata ziweze kuzisaidia timu zao. 

Alisema kuwa shirikisho hilo kupitia kamati yake ya  mashindano itasimamia kukamilifu swala la mgao wa asilimia za viingilio kwa timu hizo kwa mujibu wa utaratibu uliopangwa Ili timu hizo ziweze kujikomboa na mambo madogo madogo kama kuwalipa mishahara makocha na hata wachezaji huku ZFF ikiendelea na jitihada za kutafuta ufadhiri wa ligi kuu. 

'Mtakapohamasiha mashabiki kuja kwa wingi uwanjani hii itasaidia kupata pesa nyingi zinazotokana na viingilio vya wachezaji, tunajuana timu zetu bado maskini haina hata wale wafadhiri ambao wangeweza kuzifadhiri kwahiyo mutegemee mashabiki wenu katika kujaza uwanja"Alisema. 

Hata hivyo alisema ZFF itaendelea kuboresha ligi yake Ili iweze kuwa na mvuto wa kuwavuta mashabiki kuja kwa wingi. 

Alisema miongoni mwa6mabiresho hayo ni Bingwa kupewa kombe pamoja na Pesa taslimu Ili timu zenyewe ziweze kushindani kisoka. 

Katika ziara hiyo ambayo tayari alianza na timu a Taifa Jang'ombe inayocheza ligi daraja la kwanza Kanda pamoja na Timu ya Jang'ombe boys ya ligi kuu ya Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.