Habari za Punde

Serikali kuzilinda Taasisi za Kidini

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea vyerehani kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (wapili kushoto), vilivyotolewa  kwa  ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza  kuzitumia  katika kujiinua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi mmoja wa wananchi  cherehani zilizotolea na Taasisi ya Islamic Foundation,kulia ni  Mwenyekiti wa taasisi hiyo , Arif Nahdi,vyerehani hivyo  vimetolewa   kwa  ajili wananchi ili waweze kujikwamua  kiuchumi.
Wananchi Visiwani Zanzibar waliogawiwa vyerehani na Taasisi ya Islamic Foundation wakiwa wamesimama mbele yake baada ya kuruhusiwa kuchukua
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza  baada ya kupokea  vyerehani tisini na nne  kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (aliyekaa kulia), vilivyotolewa  kwa  ajili ya kuwagawia wananchi Visiwani Zanzibar ili kuweza  kuzitumia  katika kujiinua kiuchumi.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwandishi Wetu.
Serikali imesema itaendelea kuziunga mkono taasisi za kidini nchini ili ziweze kuleta maendeleo na kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni mdau muhimu katika maendeleo na ustawi wa  nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kupokea msaada wa vyerehani Tisini na Nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne  vilivyotolewa kwa taasisi ya TAYI  inayojishughulisha na kuwaokoa vijana kutoka katika tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
“Serikali tumekua tukipokea misaada mbalimbali kutoka katika taasisi za kidini nchini,wamekua wakisaidia visima vya maji,mashule na kubwa zaidi wanafundisha maadili ili taifa letu liwe na watu makini wanaoweza kuliletea maendeleo siku za usoni,kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani tunaahidi kuzilinda taasisi hizi ili ziweze kufanya shughuli zake bila kubughudhiwa” alisema Masauni.
Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa msaada huo wa vyerehani, Aref Nahdi  amewaomba wananchi waliopokea mssada huo kwenda kuzitumia katika shughuli za ujasirimali akiamini watapata kipato zaidi endapo watazitumia vizuri.
“Nawaomba mkazitumie vizuri ili ziweze kuwaongezea kitu kwenye vipato vyenu,natoa wito msiende kuviuza kwani lengo lake ni kuwawezesha muwe na shughuli itakayowaingizia kipato na sisi kama taasisi tunaahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa wale wanafunzi ishirini wa kwanza watakaotaka kujifunza ushonaji ili waweze kuzitumia vizuri” alisema Nahdi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopokea misaada hiyo ya vyerehani wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa vyerehani hivyo huku waiwaomba wasichoke kuwasaidia mara kwa mara ili vijana wengi wawe na shughuli za kuzalisha kipato.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.