Habari za Punde

Uzinduzi wa Kamati za Utalii za Wilaya Kisiwani Pemba leo.

Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Zanzibar  Chumu Kombo Khamis na Mkuu wa Wilaya ya Chake-chake Rashid Hadidi wakufunuwa kitambaa kuwashiria Ufunguzi wa Kamati za Utalii za Wilaya ya Pemba  katika Ukumbi wa Hoteli ya Archipelago  Kisiwani Pemba.
Naibu Waziri wa Habari  Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Chumu Kombo Khamis akimkabidhi kitabu Mkuu wa Wilaya ya Chake-chake Rashid Hadidi baaada ya Ufunguzi wa Kamati za Utalii za Wilaya ya Pemba huko Ukumbi wa Archipelago Hotel Kisiwani Pemb.
Mkuu wa Wilaya ya Chake-chake Pemba Rashid Hadidi akionyesha Kitabu cha Kamati za Utalii za Wilaya ya Pemba baada ya Uzinduzi wa Kamati Hiyo (kuliya) ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar. Abdallah Juma.
Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Chumu Kombo Khamis akitowa Maelezo kwa wajumbe waliyoshiriki katika Uzinduzi wa Kamati za Utaliii za Wilaya ya Pemba  huko Ukumbi wa Hoteli ya Archipelego (kulia) ni Katubu Mkuu Wizara ya Habari na Mambo ya kale Zanzibar Khadija Bakari Juma na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Sabaah Saleh Ali.
Wajumbe wakifuatilia Maelezo katika  Uzinduzi wa Kamati za Utalii za Wilaya Pemba uliyofanyika Ukumbi wa Hotel ya Archipelago Kisiwani Pemba.
                             Picha na Miza Othman Maelezo Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.