Habari za Punde

Shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani

Na. Hasina Khamis - Maelezo Pemba.         
AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Sanaa na Michezo Pemba, Fatma Hamad Rajab, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya kila juhudi kuona vijana wanaimarika kwa kupata ajira na kujiajiri wenyewe  ili kuweza kujikwamua na maisha yao.
Hayo aliyasema wakati Shamra Shamra ya kuanzimisha siku ya Vijana Duniani kwa kufanya usafi katika Hospital ya Chake Chake na kuzungumza na Vijana, Viongozi wa UWT na Wazazi Mkoa wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Wara Machomanne.
Mdhamini huyo aliwataka Vijana hao kuwa wazalendo na Nchi yao pamoja na kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi .
“Serikali ina dhamira mzuri  kwa vijana wake na kuhakikisha kuwa kila changamoto zinazowakabili vijana zinatatuliwa”alieleleza.
Alisema ni vyema Wazazi kuwajengea Vijana wao katika malezi yaliyo bora ili kuweza kupata Vijana wazalendo watakaolinda amani na utulivu iliyotawala Zanzibar.
Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu UVCCM Taifa, Mkoa wa kusini Pemba ,Ndugu Issa Muhammed  Kassim,aliwataka vijana kuunga mkono juhudi za Chama Cha Mapinduzi na kumpongeza Mh. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Muhammed Shein, kwa kuwaekea Wizara yao, hiyo amewataka Vijana  kuwa mstari wa mbele katika kujiletea maendeleo.
Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  Wilaya ya Chake Chake, Seif Kasim Said,alisema  Vijana wa CCM ni wakati wao wa kujitafutia elimu kwa hali zote ili kujiajiri wenyewe pamoja na kupinga Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika jamii yao.
Mwakilishi wa umoja wa vijana YUNA, Mwadini Juma Ali, alisema ni jambo la busara kwa vijana kuungana na Vijana duniani kwa kuadhimisha siku hiyo .
“Siku ya vijana ni siku adhimu kwa kuweza kumkomboa kijana "alisema.
Akitoa neno la shukurani Afisa Tiba Pemba ,Dokta Yusuf Hamad ,aliwataka Vijana kuzitambua juhudi za Serikali  kuleta maendeleo katika kila sekta ikiwemo Barabara ,Viwanda na Afya .
“Yote hayo ni kuona wananchi wanapata maisha mazuri na vijana wanapata ajira “alieleza.
Alisema vijana ndio Taifa la leo hivyo  aliwataka kuwa na moyo wa kujitolewa kwa kudumisha usafi katika maeneo ya Hospital .
Shamra Shamra za siku ya Vijana Duniani imeanza ambapo Vijana wa CCM Tawi la Wara wakishiriana na Jumuiya wa Wazazi na Wanawake, kufanya usafi katika Hospital ya Serikali na kudhamiria kafanya mambo mbali mbali ya maendeleo mpaka kufikia kilele chake  tarehe 12/8/201.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.