Habari za Punde

HESLB - TAARIFA: WAOMBAJI MIKOPO KUREKEBISHA TAARIFA

TAARIFA MUHIMU KWA WAOMBAJI MIKOPO KWA 2019/2020
Jumatatu, Septemba 23, 2019

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwajulisha waombaji wote wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa kwa sasa HESLB inaendelea na kazi ya uhakiki (verification of online-submitted applications) wa maombi yaliyowasilishwa ambayo itakamilika Jumapili, Septemba 29, 2019.

Baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki, HESLB itatoa fursa ya siku nne, kuanzia Jumatatu, Septemba 30 hadi Alhamisi, Oktoba 3, 2019 kwa waombaji mikopo ambao maombi yao yatakuwa yamebainika kuwa na upungufu kufanya marekebisho.

Taarifa hii inatolewa kufuatia HESLB kupokea maoni na maswali kupitia barua pepe na simu kuhusu hatua iliyofikiwa katika uhakiki na uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu yaliyowasilishwa HESLB.

Waombaji mikopo wote wanashauriwa kutembelea tovuti yetu (www.heslb.go.tz) au kuingia katika akaunti zao waliozoombea mkopo kupitia mfumo wa uombaji mkopo (www.olas.heslb.go.tz) kuanzia Septemba 30, 2019 ili kupata mwongozo wa kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao. Baada ya kuingia, watapata ujumbe iwapo maombi yao yamekamilika au yanahitaji marekebisho.

HESLB imejipanga kuhakikisha kazi yote ya uhakiki na uchambuzi wa maombi yote ya mikopo inakamilika ifikapo Oktoba 6, 2019 ili wanafunzi wahitaji wapangiwe mikopo, wapate taarifa na fedha za mikopo zitumwe vyuoni kabla ya vyuo kufunguliwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.hesl.go.tz).

Mwisho.

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru,
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wa-nafunzi wa Elimu ya Juu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.