Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Afungua Mkutano wa Kimataifa wa Dini Jijini Zanzibar leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Katibu wa Muungano wa Makanisa ya Evangelica kutoka Nchini Ujerumani Dr.Jochen Motte, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar, kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Kidini uluiofanyika Jijini Zanzibar. 
Baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kikristo wakisoma Dua kuanza kwa Mkutano wao wa Kimataifa wa Dini uliohusu masuala ya  amani hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu wakisoma Dua kuanza kwa Mkutano wao wa Kimataifa wa Dini uliohusu masuala ya  amani hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.    
Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa akitoa salamu kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Dini uliohusu masuala ya  amani hapo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini. 
Katibu wa Muungano wa Makanisa ya Evangelica kutoka Ujerumani Dr. Jochen Motte akitoa Taarifa ya Taasisi yao ya Kidini inavyowajibika Duniani kwenye Mkutano huo.
Katibu wa Muungano wa Makanisa ya Evangelica kutoka Ujerumani Dr. Jochen Motte akimkabidhi Taarifa ya Taasisi yao Mgeni Rasmi Balozi Seif.
Mshauri wa Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga akimkaribisha Mgeni Rasmni Balozi Seif kuufungua Mkutano huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunguaRasmi Mkutano wa Kimataifa wa Kidini hapo Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Meya wa Naispaa ya Mji wa Jakarta Nchini Indonesia Mstahiki H. Soekirman akimkabidhi zawadi ya nguzo za kiasili Mgeni rasmi Balozi Seif kwenye ufunguzi wa Mkutano huo.
Meya wa Naispaa ya Mji wa Jakarta Nchini Indonesia Mstahiki H. Soekirman na Mkewe wakimvisha nguo ya Utamaduni Balozi Seif mara baada ya kuufungua Mkutano wa Kidini huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Picha na OMPR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.