Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Masauni Awaongoza Mabalozi wa Usalama Barabarani Nchini Kuadhimisha Siku ya Mabalozi Jijini Mwanza

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia),Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi (wanne kulia), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Fortunatus Musilimu(watano kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Kamishna Msaidizi Jumanne Muliro(wapili kulia) wakiwaongoza mabalozi wa usalama barabarani na wananchi wakati wa maandamano ya amani lengo ikiwa kuhamasisha masuala ya usalama barabarrani ili kuepusha ajali za barabarani,maandamano hayo yamefanyika leo jijini Mwanza. 
Mabalozi wa Usalama Barabarani wakiwa katika maandamano ya amani yenye lengo la kuhamasisha Usalama wa Barabarani wakati wakuhadhimisha siku ya mabalozi hao iliyofanyika leo jijini Mwanza
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini  wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msadizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini  wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akipaka rangi za pundamilia katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini  wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Mwenywekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza,Ferdinand Chacha, akimwaga chenga maalumu ambazo huonyesha sehemu ya kivuko nyakati za usiku, katika sehemu ya kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la mabatini jijini Mwanza wakati wa kuadhimisha Siku ya Mabalozi wa Usalama Barabarani leo jijini Mwanza.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.