Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Amefanya Uteuzi leo.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteuwa Dkt. Zakia Mohammed Abubakar kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Dkt. Zakia anachukuwa nafasi iliyowachwa wazi na Profesa Idris Ahmada Rai ambae anamaliza muda wake wa kutumikia wadhifa huo kwa mujibu wa sheria.

Uteuzi wa Dkt Zakia umefanyika kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais, chini ya kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, namba 8 ya mwaka 1999.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee,uteuzi huo utaanzia Septemba, 06, mwaka huu.
   
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.