Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, katika mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Shein alikutana na Uongozi wa Wizara ya Nchi (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kusisitiza haja ya Idara na taasisi za Wizara hiyo kufanya utafiti ili kupata mafanikio katika malengo yake.

Alisema ni muhimu kwa viongozi wa Idara kufanya tafiti mbali mbali, akibainisha hatua hiyo itawezesha kupata maendeleo endelevu.

Aidha, Dk. Shein aliutaka uongozi wa Wizara hiyo kujenga mashirikiano na wafanyakazi wake, ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazokwamisha utendaji bora wa kazi.

Dk. Shein aliipongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake, pamoja na kuwasilisha vyema taarifa za utekelezaji wa mpango kazi kwa mwaka 2018/2019.   

Nae, akiwasilisha taarifa ya mpango kazi kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Wizara hiyo Issa Haji Ussi ‘Gavu’ alisema katika kipindi hicho Ofisi ya Rais iliendelea na ujenzi wa Ikulu ndogo Micheweni, ambapo hivi sasa imefikia hatua ya kuridhisha .

Alieleza kuwa  ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Chake chake Pemba  unaendelea vizuri,  ukitarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Aidha,  alisema  Serikali imekuwa na mahusiano mema na Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kupitia Makongamano ya kila mwaka.


Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.