Habari za Punde

Shirikisho la Soka Zanzibar Latowa Salamu za Rambirambi Kwa Familia ya Marehemu Ibrahim Jeba.


Na.Hawa Ally. Zanzibar.
RAIS wa shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar Seif Kombo Pandu ametuma salamau za rambi rambi kwa familia na ungozi wa Timu ya Chuoni kufuatia kifo  cha  mchezaji wake Ibrahimu Jeba kilichotokea hapo  hapo jana.
Jeba ambae alifariki katikam hosiptali ya Mnazi mmoja  visiwani hapa alipokuwa akipatiwa matibabu.
Katika salamu hizo Rais wa ZFF amewaomba Familia ya mpira kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao ambae Taifa bado lilikuwa likimuhitaji katika medali za soka.
Alimuelezea marehemu kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika kulitangaza soka la Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar kwa kuchezea vilabu mbalimbali vya Tanzania bara ikiwemo Mtibwa sugar, Azam Fc na hata timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars.
Aidha alisema ZFF itaendelea kukumbuka mchango wa marehemu jinsi alivyoweza  kulitumikia soka la Zanzibar hadi umauti unapomfika akiwa bado anaendelea kuitumikia timu yake ya Chuoni.
Marehemu Jeba anatarajiwa kuzikwa leo majira ya Saa saba mchana huko kijijini kwao Ndijani Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja, kifo chake ambacho kimegusa hisia kwa wadau wa soka bdani na hata nje ya Zanzibar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.