Habari za Punde

Maandali ya Uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Rubel na Polio Yakamilika

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa maelezo ya kukamilika Ufunguzi wa Mkutano kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano   itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja 
Na.Rahma Khamis Maelezo  Zanzibar. 19/9/2019
Jamii imetakiwa kuwa tayari  kuwapeleka watoto kupatiwa Chanjo ya kitaifa dhidi ya maradhi ya Surua  Rubella na Polio ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na maradhi hayo.  
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi  kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt Fadhil Mohammed Abdalla wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Wizara ya Afya .
Amesema kuwa endapo jamii itajitokeza kwa wingi  kuwapeleka watoto wao   kupatiwa chanjo hiyo itawakinga  na madhara mbalimbali ikiwemo kupoteza baadhi ya  viungo na  kupelekea ulemavu .
Aidha amefahamisha kuwa kampeni ya chanjo hiyo itazinduliwa  rasmi tarehe 26 mwezi huu  huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini A’ na zoezi hilo litaendelea kwa siku tano hadi tarehe 30 ambapo  itawalenga zaidi watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano ambao ndio waathirika zaidi wa maradhi hayo.
Nae Mkufunzi wa Kampeni ya Chanjo ya maradhi ya Surua Rubella na Polio Fathiya Saidi Bedui amesema lengo la kampeni  hiyo ni kuzuwia na kupambana na maradhi yanayozuwilika kwa chanjo .
Amesema maradhi ya  Surua na Rubella chanjo yake kuanzia  miezi 9 hadi miaka mitano  ambapo Polio kuanzia miezi 18 hadi 48 hivyo jamii iwapeleke watoto wao katika chanjo hiyo ingawa wameshawahi kupatiwa chanjo hiyo ili kupata chanjo zaidi.
Akifafanua dalili za maradhi  ya Surua  na Rubella Mkufunzi Fathiya amesema kuwa  mtoto kuwa na  homa kali kuchuruzika mafua macho kuwa mekundu na kumwaga machozi  hivyo akina mama wanapoona hali hiyo wafike katika Vituo vya Afya kwa uchunguzi zaidi.
Wakijibu maswali Mratibu wa Chanjo za mama na mtoto Yussuf  Haji Makame  na  Afisa Mipango wa Chajo Zanzibar Abdulhamid  Amour Saleh wamesema iwapo
itatokea kupooza kiungo kwa ghafla cha mtoto kufikisha Hospitali kwa haraka ili kujulikana tatizo.
Wamesema kuwa ugonjwa wa Surua na Rubella hauna chanjo maalum  hukingwa na chanjo ya Surua na Rubella hivyo ikitokea mtoto kupata maradhi hayo anatakiwa kupewa chakula na maji ya kutosha .
Wakizungumzia suala la vifaa vya chanjo hiyo wamesema  kuwa tayari vimeshakamilika na kusambazwa sehemu husika hivyo wanajamii waachane na dhana potofu na kuwapeleka watoto wao katika chanjo hiyo.
Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella na Polio itashirikisha Hospitali zote za SerIkali na binafsi na sehemu maalum ambazo zimeteuliwa kwa shughuli hiyo.
Afisa Kitengo cha Chanjo kitengo Shirikishi cha Afya ya Mama na Mtoto Abdulhamid Ameir Saleh akijibu maswali yalioulizwa  katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano   itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja .
Mkufunzi Ofisa Mpango wa Chanjo Fat-hia Said Bedui akiwasilisha mada ya Elimu ya Chanjo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Kitaifa ya Surua Rubel na Polio kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano   itakayofanyika Uzinduzi wake tarehe 26 hadi 30/09/2019 Kivunge Mkoa wa Kaskazini A Unguja 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.