Habari za Punde

Ufunguzi wa Kongamano la Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji wa Majengo Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde akishindizwa na Waziri wa Ardhi Mh. Salama Aboud Talib kufungua Kongamano la Pili la Siku ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif akisalimiana na Mrajisi wa Bodi ya Usajili, Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo Zanzibar Bibi Hawa Khamis Mzee kati kati na pembeni yao Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud.
Balozi Seif akiambatana na Waziri na Ardhi Mh. Salama Aboud pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mashmoud akitembelea Maonyesho ya Washirika wa Sekta ya Ujenzi Nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ufundi na usarifu Majengo ya Al Hatmy Bwana Abdulhamid Mhoma akimueleza Balozi Kazi mbali mbali za ujenzi zinazotekelezwa na Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ufundi na usarifu Majengo ya Al Hatmy Bwana Abdulhamid Mhoma akimueleza Balozi Kazi mbali mbali za ujenzi zinazotekelezwa na Kampuni hiyo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Vifaa vya Huduma ya Maji safi na salama kutoka Ujerumani ya RAK therm yenye Tawi lake Zanzibar akimfahamisha bidhaa zao zilizoko kwenye soko.
Balozi Seif pamoja na Viongozi wenzake akimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa Kampuni ya OTIS iliyoshiriki maonyesho kwenye Kongamano la Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo Zanzibar.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Salama Aboud Talib akijiandaa kumkaribisha Balozi Seif kulifungua Kongamano la Pili la Siku ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde.
Washirika wa Sekta ya Ujenzi wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi   akilifungua Kongamano la Pili la Siku ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Salama Aboud Talib akijiandaa kumkaribisha Balozi Seif kulifungua Kongamano la Pili la Siku ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo katika Ukumbi wa Hoteli ya Verde.
Mrajisi wa Bodi ya Usajili, Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo Zanzibar Bibi Hawa Khamis Mzee akimpatia maelezo Balozi Seif juu ya matengenezo ya zawadi aliyotunukiwa Rais wa Zanzibar na Wasanufu wa Ujenzi Zanzibar.
Balozi Seif akiwakabidhi vyeti baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Mbweni mara baada ya kulifungua Kongamano la Pili la Siku ya Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.