Habari za Punde

Vijana Watakiwa Kuyatumia Vizuri Mafunzo Wanayopatiwa

Na. Masanja Mabula Pemba.
MRAJIS wa Tasasi zisizo za kiserikali Ndg.Ahmed Khalid Abdalla amewataka Vijana waliopatiwa mafunzo ya ujasiriamali kuyatumia vyema ili kuleta mabadiliko kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amesema serikali imeweka mazigira bora na wezeshi kwa vijana , hivyo ni vyema  kuzitumia fursa za mafunzo zinazotolewa na Serikali na taasisi binafsi.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 30 wa shehia ya Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni yaliyofanyika katika katika ukumbi wa  mikutano wa redio Jamii  , Ahmed amesema  mafunzo hayo yatawakomboa vijana na kuwafanya waweze kujiajiri wenyewe.
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana mchango wa asasi za kiraia  katika kuchagia uchumi wa nchi na wananchi wake, hivyo itaendelea kuziunga mkono asasi zinazolenga kuwaondoa vijana kutoka giza la umaskini” alifahamisha.
Aidha Mrajisi ameitaka Jumuiya ya TUDOPE kuendelea kuwakusanya vijana na kupata elimu ya ujasiriamali pamoja na elimu ya stadi za maisha ambayo itawaongezea ubunifu katika kujiletea maendeleo.
Akifungua mafunzo hayo ya siku mbili, Mweyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni Mariam Omar Ali amesema uwepo wa mafunzo hayo kwa vijana  ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya 2015-2020.
Amewataka vijana hao kutojihusisha na masuala ya kisiasa wakati wanapotekeleza shughuli zao ,kwani siasa ni sumu ya maendeleo na inaweza kusambaratisha umoja wao.
“Katika ilani ya uchaguzi wa CCM ya 2015-2020, suala la kuwapatia elimu ya ujasiriamali vijana limeelezwa , hivyo mafunzo haya ni utekelezaji wa ilani” alifahamisha.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mchanga Khamis Hamad amesema kwamba , mafunzo hayo yamekujawakati muafaka la kuahidi kuyatumia kama ilivyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.