Habari za Punde

Wakufunzi wa Mchezo wa Mpira wa Kikapu Kutoka USA Watowa Mafunzo ya Mchezo huo Kwa Vijana Chini ya Miaka 18 Zanzibar.A

Mchezaji wa zamani wa mpira wa Kikapu wa NBA Nchini Marekani Jim Cleamons akitowa mafunzo ya mchezo huo kwa Wachezaji mbalimbali wa Timu za Mpira wa Kikapu Zanzibar walio na umri wa chini ya miaka 18, mafunzo hayo yamefanyika katika Uwanja wa Ndani wa Basketi Ball Mao Zedong Zanzibar. 
Kocha wa Mpira wa Kikapu Nchini Marekani mchezaji wa zamani wa ligi ya NBA Jim Cleamons akitowa mafunzo ya mchezo kwa Vijana wa chini ya miaka 18 kutoka timu mbalimbali za mchezo huo wakipata mafunzo hayo yaliofanyika katika Uwanja wa ndani wa Ma0o Zedong Zanzibar. 
Mchezaji wa zamani wa Mpira wa Kikapu Vyuo Vikuu vya Marekani kwa sasa ni Kocha wa mchezo huo Chineze Nwagbo akitowa mafunzo hayo kwa Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Kikapu Zanzibar walio chini ya umri wa miaka 18 mafunzo hayo yamefanyika katika uwanja wa ndani wa Mao Zedong Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.