Habari za Punde

Maandalizi ya Kiwanja cha Amani Ambacho Kinatarajiwa Kutumika kwa ajili ya kufanyika Shehe za miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.


Mounekano wa haiba nzuri inayopendeza ya Uwanja wa Michezo wa Aman ukiwa katika matayarisho ya mwisho huduma ndiogo ndogo za matengenezo ili kukidhi Kilele cha maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaabani Seif pamoja na Mohamed Katibu Mkuu wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Omar Hassan Omar ( Kingi) wakiukagua Uwanja wa Michezo wa Amani kujiridhisha kwa ajili ya ufanikishaji wa Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi kutimia Miaka 56.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Nd. Mussa Ramadhan Kushoto akitoa maelezo baada ya juhudi kubwa iliyofanywa na Wahandisi wa ZAWA ya kufanikisha upatikanaji wa Huduma za Maji safi na salama kwenye Uwanja huo.

Watendaji wa taasisi mbali mbali  za serikali zinazohusika na kutoa huduma kwa ajili ya kufanikisha sherehe za Mapinduzi wametakiwa kufanya kazi kwa mashirikiano ili kufanikisha sherehe za miaka 56 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar zinazotarajiwa kufanyika Januari 12, 2020.
Mashirikiano hayo yatazidi  kusaidia kufanikisha sherehe hizo kufanyika kwa ufanisi ikiwa ni sehemu ya kuenzi kumbukumbu ya historia ya Zanzibar iliyowakomboa wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba kwa kupata uhuru wa kweli katika Nyanja mbali mbali ikiwemo Uchumi, Elimu na Kijamii.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Shaabani Seif Mohamed alieleza hayo wakati akikagua maendeleo ya maandalizi ya Kiwanja cha Amani ambacho kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kufanyika Shehe za miaka 56 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Alieleza kuwa kutokana na maandalizi yaliofikiwa kwa mashirikiano ya karibu kati ya Idara ya Sherehe na Maadhimisho ya shughuli za kitaifa iliyo chini ya Ofisi ya makamu wa pili wa Rais na taasisi nyengine za serikali yamesaidia kufanikisha maandalizi ya kiwanja hicho na hakuna shaka yoyote juu ya matumizi ya Kiwanja kwa sherehe zinazotarajiwa.
Akizungumiza suala la upatikanaji wa huduma muhimu katika kiwanja hicho ikiwemo  huduma ya Umeme na maji  safi na salama Katibu Mkuu Shaaban ameonesha kuridhishwa kwake kutokana na mikakati na jitihada imara zilizochukuliwa na uongozi wa mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) kwa kuisogeza karibu huduma hiyo na kufanikisha kuweka maji mengine ya akiba endapo yatahitajika wakati wowote.
“Niseme tu Nawapongeza sana ndugu zangu wa mamlaka ya maji Zanzibar kwa ushirikiano wao mzuri walioutoa katika kuhakikisha huduma hii muhimu inapatikana kiwanjani hapa katika kipindi chote cha sherehe” Alieleza Katibu Mkuu
Akitoa maelezo Katibu Mkuu wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Omar Hassan Omar ( Kingi) alimueleza Katibu Shaaban kuwa maandalizi ya uwanja huo tayari yamekamilika hadi kufikia Asilimia 80%  kwa kufanya marekebisha sehemu ya uwanja ikiwemo kuweka alama ndani ya kiwanja zitakavyoviwezesha vikosi vya Ulinzi na usalama kucheza gwaride bila ya usumbufu.
Aidha, alisema Wizara inajitahidi kuhakikisha usafi wa mazingira ya nje na ndani ya uwanja huo yanakuwa yenye haiba nzuri yenye kuvutia huku mafundi wengine wakiendelea kukamilisha baadhi ya mambo yanayohitajika kiwanjani hapo.
Wakati wakiendelea kukikagua kiwanja hicho Katibu Mkuu Shaabani Ametoa wito kwa mafundi waliopewa dhamana ya kurekebisha maeneo mbali mbali ya kiwanja hicho kuhakikisha wanafanikisha majukumu waliokabidhiwa ndani ya wakati waliopangiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.