Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifungua mashindano ya pili
ya mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15
Disemba, 2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi yake
ni mdhamini wa mchezo wa Taekwondo akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya
mchezo wa Taekwondo yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 14-15 Disemba,
2019 mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana
Shonza na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo Tanzania (TTF) Ramoudh Ally
(kulia).
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha
Serikali
ya Awamu ya Tano imeipa kipaumbele sekta ya michezo nchini kwa kuweka mikakati
inayohakikisha michezo yote ikiwemo Taekwondo inafanya vizuri ili kuwa chanzo
cha kutoa ajira kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa taifa.
Akifungua
mashindano ya Taekwondo ya pili ya mchezo wa yanayofadhiliwa na Ubalozi wa Korea
nchini kwa mwaka 2019 kwa nchi za Afrika ya Mashariki yanayofanyika katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mw wiki, Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa michezo yote
nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo.
Akijibu
moja ya maombi yaliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo nchini
(TTF) Ramoudh Ally la kupatiwa eneo la kujenga uwanja mkubwa wa ndani wa kisasa
kwa ajili ya mchezo wa Taekwondo wakati akitoa historia ya mchezo huo nchini,
Naibu Waziri alisema kuwa kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya michezo nchini
ya mwaka 1995 jukumu la kusimamia na
kuendeleza sekta ya michezo ni la Serikali, jamii nzima pamoja na wadau
mbalimbali ukiwemo Ubalozi wa Korea nchini.
“Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendelea
kushirikiana na Serikali kukuza, kuendeleza na kuwekeza katika sekta ya michezo
nchini ikiwemo mchezo wa Taekwondo, kwani Serikali ipo tayari kushirikiana na
wadau mbalimbali kuendeleza michezo ikiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea
nchini ili kuhakikisha sekta hii inakuwa na tija kwa jamii na taifa zima”
alisema Naibu Waziri Shonza
Aidha,
ameataka maafisa michezo nchini kuanzia ngazi ya mikoa na wilaya kushirikiana
na viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo ili kuhakikisha vyama na
vilabu ambavyo havijapata usajili kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT) ambalo
limepewa dhamana ya kusajili mashirikisho, vyama na vilabu hapa nchini.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Korea nchini Cho Tae-ick ambaye ofisi
yake ni mdhamini wa mchezo huo amesema kuwa mchezo wa Taekwondo unafaida nyingi
na unachezwa na watu wa rika zote kuanzia watoto wadogo hadi watu wazima kwa
kuimarisha na kujenga mwili ambapo husaidia kuimarisha umakini katika kutimiza
majukumu yao ya kila siku.
Balozi
huyo ameendelea kuzitaja faida nyingine za mchezo huo kwa ni kuwajengea uwezo
wachezaji wa kujilinda kiusalama, kuwafundisha saikolojia ya namna bora ya
maisha pamoja na kuwajengea urafiki miongoni mwa wachezaji.
“Taekwondo
ni mchezo mzuri sana, kila kitu katika mwili wa binadamu ni silaha ya
kujikinga, cha msingi ni kujua namna ya kuitumia kwa faida kwa jamii nzima,
elimu hiyo inapatikana katika mchezo wa Taekwondo” alisema Balozi Cho.
Awali
akitoa historia ya mchezo wa Taekwondo nchini Rais wa Shirikisho la mchezo huo
nchini (TTF) Ramoudh Ally alisema kuwa Taekwondo ni mmoja kati ya michezo
inayotambuliwa na Baraza la Michezo Tanzania pamoja na Kamati ya Olympic
duniani.
Mchezo
Taekwondo nchini ulianza kutambuliwa rasmi mwaka 2003 na Shirikisho la
Taekwondo duniani ambalo makao yake makuu yapo nchini Korea ya Kusini ambapo
hadi sasa Tanzania ni mwanachama hai na inashughulika na masuala yote ya mchezo
huo duniani.
Mashindano
Taekwondo ya mwaka 2019 yanayojulikana kama “Korean Ambassador’s Cup” ni ya
pili kufanyika nchini ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili kwa mara ya kwanza
yalifanyika mwaka 2017. Mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa siku mbili
kuanzia tarehe 14 hadi 15 Disemba 2019 jijini Arusha ambayo yanajumuisha jumla
ya washiriki 172 kutoka katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda,
Uganda na mwenyeji Tanzania pamoja na washiriki kutoka nchini Malawi.
No comments:
Post a Comment