Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein Atembelea Maonesho ya Wajasiriamali Kabla ya Kufungua Kongamano la Sita la Diaspora Tanzania Lililofanyika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar leo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira.Mhe.Goerge Simbachawene, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar kuhudhurua hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Sita la Diaspora Tanzania lililofanyika Zanzibar, kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Issa Haji Gavu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi. Ramadhan Muombwa Mwinyi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Issa Haji Gavu alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar kuhudhurua hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Sita la Diaspora Tanzania lililofanyika Zanzibar, kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi. Ramadhan Muombwa Mwinyi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora.Ndg.Norman Jasson alipowasili katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar kuhudhuria hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Sita la Diaspora Tanzania lililofanyika Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi wakipata maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Kibibi Product kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi hicho Bi. Prisca Kataya 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na moja ya bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Donge Pwani, wakati akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Zanzibar katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Diaspora Tanzania lililofanyika katika Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.