Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akitembelea mabanda ya
wafanyabiashara wa sanaa za ufundi wanaoendesha shughuli zao katika kijiji cha
mwenge vinyago katika ziara yake ya kikazi katika eneo hilo,(wa kwanza kulia)
Katibu Mkuu wa Chama cha wachonga vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi
akiwahahihishia na wafanyabiashara wa
Sanaa ya ufundi na wachongaji wa vinyago
wanaofanya shughuli zao katika kijiji cha mwenge vinyago leo jijini Dar es
Salaam kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro wa eneo hilo ndani ya mwaka
2020 alipotembelea eneo hilo kwa ajili
kuwataka kuacha kutofautiana kwani hilo ndiyo linalokwamisha kumalizika
kwa mgogoro huo.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa
kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo akiwahakikishia
ushirikiano kutoka wizarani wachongaji wa vinyago na wafanyabiashara wa sanaa
ya ufundi wanaoendesha shughuli zako katika eneo la kijiji cha mwenge vinyago
alipowatembele jana katika eneo hilo jijini Dar es Salaam,(wa kwanza kulia)
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi.
Rais wa Shirikisho la
Sanaa za Ufundi Tanzania Bw.Adrian
Nyangamale akiomba viongozi wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa tamko la kulitaka Baraza la Sanaa la
Taifa kutoa mwongozo wa kusimamima uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika
eneo Kijiji cha Mwenge vinyago Jijini Dare s Salaam,walipotembelewa na
viongozi wa Wizara hiyo,(wapili kulia) Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi.
Baadhi ya wasanii wa
kuchonga vinyago na wafanyabiashara wa sanaa ya ufundi wanaoendesha shughuli
zao katika eneo mwenge vinyago wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (aliyeketi
wanne kutoka kulia)mara baada ya kikao na wadau hao katika eneo hilo,(watatu
kushoto) Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Bibi.Joyce Fisoo na (wakwanza kulia aliyeketi) Rais wa Shirikisho la Sanaa za
Ufundi Tanzania Bw.Adrian Nyangamale.
Na.Anitha Jonas –
WHUSM,Dar es Salaam.31/12/2019.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amewahikikishia
wasanii wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mwenge Vinyago kuwa serikali
itahakikisha inamaliza mgogoro wa eneo
hilo ndani ya mwaka 2020.
Dkt.Possi ametoa
kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea eneo hilo la wachogaji wa vinyago na wauzaji wa kazi za sanaa za
ufundi lilopo Mtaa wa Nzasa kata ya
mwenge kwa lengo la kufahamu ukubwa wa eneo hilo pamoja na kuzungumza na wadau
wanaoendesha shughuli zao eneo hilo na kufahamu changamoto zao.
“Eneo hili ni kubwa
na nieneo la kimkakati kabisa kuendesha biashara zenu hivyo serikali imedhamiria
inatatua kero yenu ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi hii uliyodumu kwa miaka mingi
kwani ili kila mmoja wenu aweze kuendesha shughuli zake za kujipatia kipato na
hata atakapopatikana mwekezaji basi aweze kuwa huru kuwekeza na kuboresha miundombinu ,“alisema Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza
katika kikao hicho na wadau hao Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwasahii wadao hao
kuacha kuwa na makundi na kutofautiana kwani migogoro hiyo ndiyo
itakayokwamisha kukamilika kwa kutatuliwakwa kero za eno hilo hivyo wawe wamoja
na waache kumfuatisha huyo anayewajengea chuki miongoni mwao na kuleta
mgawanyiko.
Aidha, nae Katibu wa
Chama cha Wachogaji wa Vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani alitoa ombi la mazingira
ya eneo hilo kuboreshwa katika suala la ulinzi,usafi kwani itasadia wasanii wachongaji wanaofanya
shughuli zao kuzifanya kwa ufanisi zaidi na kuongeza ubunifu ambao utalitangaza
taifa vyema.
“Ukosefu kwa mafunzo stadi za sanaa ya
uchongaji wa na uhaba wa vitendea kazi vya kisasa umekuwa ni kero ya
inayokwamisha maendeleo ya kazi hii,”alisema Bw.Ramadhani.
Pamoja na hayo Katibu
Mkuu huyo wa CHAMUSATA alitoa maombi ya
kwa BASATA kutoa tamko juu ya mwongozo
wa matumizi ya eneo hilo sababu ndiyo waliyokabidhiwa kusimamia eneo hilo kwa
tamko la Mheshimiwa Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe tangu mwaka 2018.
Halikadhalika kwa upande wa Mhasibu Mkuu wa
Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Onesmo Kayanda aliyemuwakilisha Katibu Mtendaji wa
Baraza hilo aliahidi kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu
huyo maara baada ya risala ya chama cha wachongaji vinyago Tanzania kusomwa.
No comments:
Post a Comment