Habari za Punde

TAASISI YA HUDEFO NA WADAU MBALIMBALI WA MAZINGIRA WAFANYA USAFI UFUKWE WA MSASANI


Taasisi isiyo ya Kiserikali ya HUDEFO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanamapenzi ya mazingira wamefanya usafi katika ufukwe wa Msasani ikiwa ni sehemu yao ya kufanya hivyo kila mwezi. Mratibu wa zoezi hilo Bi.Sarah Pima alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa sababu wananchi wenyewe ndio haswa watumiaji wa ufukwe huo wa bahari, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha inakuwa safi kila wakati.
 Hali ya taka ngumu ilivyokuwa kabla ya kuanza usafi wa ufukwe wa bahari, ambapo pameonekana kuwa na tatizo kubwa hasa katika chupa za plastiki zenye rangi kusambaa bila kuokotwa kwa sababu hazina dili lolote kwa wale waokota makopo, hii inapelekea kuchafua bahari kwa kasi.
 Wadau mbalimbali wakiendelea kusafisha ufukwe wa Msasani
 Moja ya kikundi cha wakimbiaji ambao hutumia pia ufukwe huo wa Bahari kwa ajili ya mazoezi yao ya kila wakati wakiwa wanafanya usafi
 Wanafunzi kutoka Chuo cha NIT ambao wanapenda mazingira wakiwa wameungana na wadau wengine kuendelea kufanya usafi
 Mratibu wa zoezi la usafi wa ufukwe wa Msasani Bi. Sarah Pima (aliyevaa buti la kijani) akitoa maelezo kwa wadau wa mazingira namna bora ya kukusanya taka hizo.
 Ukusanyaji wa taka ngumu na zile ambazo zinaoza ukiwa unaendelea
 Kujali Afya ni muhimu hapa washiriki wa usafi wakiwa wanapewa vitendea kazi
 Wadau wa mazingira kwa uwezo wao wakiwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa taka ngumu ambazo ni tatizo katika bahari
 Baadhi ya taka ngumu ambazo zimeokotwa tayari kwa ajili ya kwenda kutupwa eneo maalum
 Baadhi ya wanachuo kutoka UDSM wakiwa wanaendelea na usafi
 wadau wa mazingira wakiwa wanachimba mashimo ili kufukia taka ambazo zinaweza zikaoza
 Hawa ni wadau wa mazingira ambao walifanikisha kwa kiasi kikubwa kufanya usafi katika ufukwe wa msasani.

(Picha zote na Fredy Njeje - Mdau wa Mazingira)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.