Habari za Punde

Uzinduzi wa Programa ya Ajira Kwa Vijana Zanzibar, Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar. kuhudhuria hafla ya Uzinduzi na Utekelezaji wa Program ya Ajira kwa Vijana  Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar.Ndg. Omar Hassan King akitowa maelezo ya kitaalam ya baadhi ya Vifaa Kazi vitakavyokabidhiwa Vijana, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Utekelezaji wa Programu ya Ajira kwa Vijana Zanzibar. 


WAZIRI wa Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Ajira kwa Vijana Zanzibar, hafla iliofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi,  akiwahutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Programu ya Ajira kwa Vijana Zanzibar , iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijin i Zanzibar.
VIJANA na waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi na Utekelezaji wa Program ya Ajira kwa Vijana, hafla iliofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abduwakili Kikwajuni
MAKAMU wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Utekelezaji wa Program ya Ajira kwa Vijana, (kulia) ni Waziri  wa Vijana Sanaa na Michezo, Balozi Ali Karume
MAKAMU wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi cherehani Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Hamida Issa, kwaajili ya kuwapatia Vikundi vya Vijina vilivyomo ndani ya Wilaya zao, hafla iliofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abduwakili Kikwajuni

VIJANA na waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi na Utekelezaji wa Program ya Ajira kwa Vijana, hafla iliofanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abduwakili Kikwajuni
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na wa Wizara ya Vijana Michezo Utamaduni na Sanaa baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Utekelezaji wa Programu ya Ajira kwa Vijana Zanzibar, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini  Zanzibar.
 (Picha na Abdallah  Omar.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.