Habari za Punde

Katibu Mkuu TIXON Aongoza Kikao Cha Kujadili Ujenzi wa Wajengo ya Ofisi za Wizara Awamu ya Pili Eneo la Mtumbani.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akizungumza neno la ufunguzi wakati wa kikao kazi cha wadau wa ujenzi walipokutana Januari 27, 2020 kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.Kikao kilifanyika katika Ukimbi wa Mkutano wa ofisi yake Dodoma, wa kwanza kushoto ni Katibu wa kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha wadau wa ujenzi walipokutana Januari 27, 2020 kujadili mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Sehemu ya  wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali kwa Awamu ya Pili wakifuatilia hoja za kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali kwa Awamu ya Pili wakifuatilia hoja za kikao hicho.
Wajumbe wa kikao cha kujadili mpango wa ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara kwa Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakifuatilia hoja za Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi Idara ya Ushauri kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Wencelaus Kizaba akiwasilisha taarifa ya mpango wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara kwa Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu, Januari 27, 2020.
 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.