Mchezaji wa Timu ya Jamuhuri Khalfan Abdalla akimpita beki wa Timu ya JKU Mwinjuma Mwinyi wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa bao.1-0.
MAAFANDE wa timu za Soka za Jeshi la Kujenga Uchumi JKU imefanikiwa kuifunga Timu ya Jamuhuri katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.
JKU ilishinda bao 1-0 dhidi ya Timu ya Jamhuri katika mchezo wao uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong
Timu ya JKU imeandika bao lake la kwanza na la ushindi kupitia mchezaji wake Suweid Juma dakika ya 73 ya mchezo huo katika kipindi cha pili.
Ushind wa JKU unaifanya kuendelea kuwa Katika nafasi yake ya tatu kwa kufikisha pointi 25 katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KMKM wenye pointi 27, wakati KVZ kwa matokeo hayo KVZ wamefikisha point 18 na kupanda nafasi moja kutoka wa Saba hadi wa sita na kuwashusha Mafunzo ambao wana point 15.
Aidha katika uwanja wa Amaan timu ya Zimamoto ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mlandege .
Zimamoto Katika mchezo huo ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 10 tu kupitia kwa mchezaji wake Hamad Ibrahim Hilika alilolifunga kwa mkwaju wa penanti.
Mlandege kufungwa kwao huko hakukuawafanya wapote mwelekeo na badala yake walijirekebisha makosa yao na kufanikiwa kusawazisha ndani ya dakika ya 81 kupitia kwa Yahya Karoa.
Beki wa Timu ya JKU akimpita mchezaji wa Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa bao.1-0.
No comments:
Post a Comment