Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Wahitimu wa kidatu cha nne wametakiwa wasitosheke na ufaulu waliupata waongeze bidii katika masomo yao wanayoendelea ili kufikia malengo yao ya baadae .
hayo aliyasema Dkt.Abdalla Ismail Kanduru katika Mahafali ya Skuli ya Sunni Madressa Mkunazini wakati akikabidhi vyeti kwa wahitimu waliomaliza masomo yao ya kidatu cha nne .
Amesema licha ya matokeo mazuri yaliyopatikana wanafunzi wazidishe juhudi katika masomo yao yan kidatu cha tano kwa mustakbali ya maisha yao ya baadae.
Amesema wanafunzi wengi hivi sasa wanashawishika kuingia vyuoni na kukataa kusoma kidatu cha tano na sita jambo ambalo sio sahihi kwani kila siku sifa zinabadilika za kuingia Chuo Kikuu .
“Kila siku mambo yanabadilika nashauri yule alifanikiwa kuingia kitatu cha tano aendelee waache kukimbilia kwenye vyuo jambo ambalo sio njia sahihi ya uwamuzi”.alisema Dkt Kanduru .
Alifahamisha kuwa wanafunzi walihitimu masomo yao wasijibweteke hata kama wazee wao watakuwa na uwezo lazima wazidishe juhudi za kujitafutia maendeleo yao wenyewe katika maisha yao ya baadae.
Aidha aliwataka walimu na walezi kuzidisha mashirikiano katika usimamizi wa wanafunzi wao kwa lengo la kuongeza juhudi za ufundishaji na kuimarisha ongezeko la ufaulu wa wanafunzi hao
Nae Mwakilishi wa Rais wa Jamat Murtaza Turk alisema juhudi za walimu na walezi wa wanafunzi pamoja na wajumbe wa bodi ya skuli hiyo zimeweza kusaidia ufaulu mzuri wa skuli hiyo .
Alifahamisha kwamba katika wanafunzi 70 wa kidatu cha nne waliofanya mitihani yao, wanafunzi 10 wamepata devition 1 ,13 devition11 , 22 devition 111 na 25 ni devition 1V wameweza kufuta sero kwa mwaka huu jambo ambalo ni faraja .
Aidha alisema kipindi cha mwaka jana kulikuwa na changamoto kubwa kwa wanafunzi kutofauli vizuri jambo ambalo lilichafua sifa nzuri ya skuli hiyo .
No comments:
Post a Comment