Habari za Punde

MASAUNI ATEMBELEA CHUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHOGO NA KUFANYA MKUTANO NA WAKIMBIZI RAIA WANAOLALAMIKIA KUPORWA ARDHI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe (watatu kulia),Mbunge wa Handeni Vijijini,Mboni Mhita(kushoto) na   Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo ,Kamishna Msaidizi,Kennedy Komba(kulia), wakipita katika moja ya mabweni yanayojengwa katika chuo wakati wa ziara ya naibu waziri leo kukagua ujenzi  wa mabweni  wilayani Handeni mkoani Tanga
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo ,Kamishna Msaidizi,Kennedy Komba(kulia) wakati wa ukaguzi wa mabweni yanayotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga,leo.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani),wakati wa kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya naibu waziri kuwasili wilayani Handeni leo  kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Handeni,mkoani Tanga leo baada ya kuwasili katika kijiji cha Chogo kwa ziara ya kikazi.Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Godwin Gondwe
Mkazi wa Kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku,Sharrif Abdul akimpiga picha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani),wakati akitoa maelekezo ya Serikali juu ya mgogoro wa ardhi unaohusisha Wakimbizi kutoka nchini Somalia waliopewa uraia mwaka 2004 na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.Naibu Waziri Masauni amefanya mkutano wa hadhara leo,wilayani Handeni kusuluhisha mgogoro huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.