Habari za Punde

Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Nchi Wanachama wa SADC .

Naibu Katibu Mkuu Nchi wanachama jumuiya ya SADC  Dkt,Thembinkosi Mhlongoi akizungumza katika Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar.

Na.Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar 18/02/2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Uwekezaji Doroth Mwaluko amesema kufanyika Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC) kutasaidia kubadilishana taarifa za uzoefu pamoja na kupunguza athari za Maafa .
Hayo aliyasema wakati wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi huko katika Ukumbi wa Madinat Al- Bahr Mbweni Zanzibar
Alisema kikao hicho kitasaidia kuwa na jukwaa la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kwa lengo la kutekeleza kwa ufanisi shughuli za usimamizi wa maafa
Aidha alisema Mkutano huo umekuja katika kipindi ambacho nchi nyingi wanachama katika ukanda huu zimekuwa zikiathiriwa na majanga ya asili ya mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa .
Nae Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Abdalla Hassan Mitawi amezishauri Nchi wanachama wa SADC kushirikiana katika kukabiliana na maafa kwa hatua watazozichukua ili kudhibiti athari za kimazingira zinazoweza kujitokeza.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari inatumia boti za uokozi pamoja na ndege zisizokuwa na rubani kwa kuimarisha shughuli za uokozi hata hivyo inahitaji ushirikiano unahitajika kutoka Nchi nyengine.
 Mkutano huo wa Ngazi za Makatibu Wakuu unaandaa Ajenda zitazojadiliwa katika Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufunguliwa siku ya Ijumaa ijayo na Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ni Rais wa ZanzIbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein katika Hoteli ya Madinat Al Bahr
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “USHIRIKI WA KISEKTA KWENYE KUPUNGUZA MADHARA YA MAAFA NI NJIA BORA YA KUIMARISHA USTAHAMILIVU KATIKA UKANDA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA” ( SADC)

 Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya uongozi wa  Maafa kwa Nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa  Nchi Wanachama 15 kati ya 16 zitashiriki Mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Abdalla Hassan Mitawi akitoa hotuba  katika Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Uwekezaji Doroth Mwaluko akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya maafisa Waandamizi waliohudhuria katika Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar
Makatibu Wakuu na maafisa Waandamizi wakiwa katika Picha ya pamoja katika hafla ya  Ufunguzi wa Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Abdalla Hassan Mitawi akizungumza na Waandishi kuhusiana na Mkutano wa Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kubadilishana taarifa za uzoefu na upunguzaji wa Athari za maafa kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC uliofanyika Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.