Habari za Punde

Wanawake Watakiwa Kujitokeza Katika Zoezi la Uandikishaji na Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapika Kura.

Na Takdir Suweid Maelezi Zanzibar.
Akinamama wa UWT wametakiwa kushiriki katika zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura ili waweze kuchaguwa Viongozi watakaotetea maslahi yao.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi Tauhida Cassian Galos amesema kupiga kura ni haki ya kila mtu wenye sifa hivyo ni vyema kuhamasishana kushiriki katika Daftari hilo ili waweze kuwa na sifa za kupiga kura.
Akizungumza na Watendaji wa Uwt Wilaya ya Mfenesini Kichama kuhusiana na Daftari la kudumu la Wapiga kura linaloendelea huko Dole Wilaya ya Magharibi ‘A’ amesema wakati umefika wa kuchaguwa Viongozi watakaoweza kuwatatulia matatizo yanayowakabili iliwemo Umasikini,Udhalilishaji,Ajira na uhaba wa Fedha za kuanzisha miradi ya Maendeleo.
Amesema iwapo Wananchi watajitokeza kupiga kura kutaiwezesha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kuendelea kubaki Madarakani na kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali  za kiuchumi kwa jamii na Taifa kwa Ujumla.
Aidha amewataka Wanawake kuendelea kuitunza na kuilinda amani ya nchi iliopo ili Serikali izidi kutekeleza mipango ya maendeleo ilojipangia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.