MKUU wa wilaya ya Tanga Ndg.Thobias
Mwilapwa kulia akizungumza wakati akishukuru Taasisi ya Odo Ummy
Foundation kwa msaada ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya
kuwekea
ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na
maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia katikati
ni Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga
Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy
Foundation Ndg.Khatibu Kilenga kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
Tanga Ndg.Thobias Mwilapwa kushoto kabla ya kuona msaada
ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea
ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na
maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia ambayo
vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa nyumba za ibada
misikiti na makanisa Jijini Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga Ndg.Thobias
Mwilapwa kushoto akiangalia koki zilizopo kwenye ndoo hizo ambazo
zilitolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa
kwenye misikiti na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa
wa Corona.
Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa na
Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa kwenye misikiti
na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona.
Na.Mwandishi Wetu - Tanga.
TAASISI
ya Odo Ummy Foundation ya Jijini Tanga imetoa msaada wa vifaa vya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa taasisi za dini
zilizopo Jijini humo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanaepukana na
maambukizi hayo kwa kuchukua tahadhari.
Msaada uliotolewa ni
ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ili
kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo
ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisa dunia.
Akizungumza wakati
wa halfa hiyo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias
Mwilapwa, Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga
ambayo ilianzishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ikiwa na
lengo l kujenga hamasa kwenye jamii na kusaidia masuala mbalimbali ya
kijamii.
Alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikiwasaidia kwenye
mambo mengi ikiwemo elimu,afya na makundi madogo madogo ya kijamii
ikiwemo vijana na wanawake ili kuweza kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi
kupitia fursa zilizopo kwenye maeneo yao na hivyo kuharakisha maendeleo.
“Kwenye janga hilo lililoikumba dunia la Corona hatukuwa nyuma
tumeona angalu tutoa ndoo na sabuni kwa ajili ya kusaidia kupunguza
maambukizi ambao yanaonekana kukua kwa kasi kwenye maeneo mbalimbali
lakini pia ni sehemu ya kutoa elimu pamoja na kwamba kuna maelekezo
mbalimbali yanayotolewa ya kujilinda kwa kunawa mikono vizuri pamoja na
kutumia maski ”Alisema
Aidha alisema wao wameona wagawe ndoo 60
maana ya zenye maji na za kukingilizia 60 hivyo kufikia ndoo 120 na
vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ambayo watazigawa kwenye maeneo ya
misikitini na kanisani ambapo wameona kutakuwa na uhaba mkubwa.
“Katika
maeneo ya ibada misikitini na kanisani tuliona vifaa hivyo
havijawafikia na ndio maana tuliona tusambaze huku akisisitiza kwamba
hiyo ni hatua ya kwanza ya kusaidia jambo hilo lakini hapo mbeleni
wanakusudia kufanya jambo mkubwa zaidi”Alisema Kilenga
Hata
hivyo alisema pia wataendelea kuchangia mambo mbalimbali kwa jamii kwani
matatizo yao ni yetu na hivyo ndio kauli mbiu ya Taasisi yetu kwamba
“Tanga yetu ni wajibu wetu” huku akimkaribisha Mkuu huyo wa wilaya
ashiriki nao katika kuliunga mkono jambo hilo akiwa kama msimamikzi mkuu
wa wilaya.
Awali akizungumza wakati wa alipotembelea na kuona
vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliishukuru Taasisi
ya Oddo Ummy Foundation na Mbunge Ummy kwa kuja na mpango huo wa
kusaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka ambapo kwa sasa
wamekuwa wakikabiliana na ugonjwa wa Corona.
Alisema ni faraja
kubwa kwa kuja na mpango huo wa kutusaidia watu wa Tanga vifaa hivyo
kufanyia jambo la usafi ambalo ni sharti la umuhimu katika mapambano
dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
“Lakini nishukuru Taasisi
ya Oddo Ummy foundation kuianisha msaada huo ujieleze kwenye maeneo
gani hilo ni jambo la msingi sana na muhimu hivyo tunakushukuru sana kwa
hili ambalo umelifanya kupitia Taasisi yenu na tunafurahi kuona
umeelekeza hili liende kwenye jumba za ibada”Alisema
Aidha
alisema kwamba wamefurahi sana kuona msaada huo uelekezwe kwenye nyumba
za ibada na itakuwa ni mchango mkubwa sana kwao kuweza kuimarisha
jitihada mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ambao ni hatari
duniani.
“Msaada huo umekuja kutupa nguvu kwa juhudi ambazo
tumekuwa tukizifanya hivyo tunakushukuru sana huku akizitaka taasisi za
dini ambazo zitanufaika na msaada huo kuhakikisha wanavitumia kwenye
matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo “Alisema DC Mwilapwa.
No comments:
Post a Comment