Habari za Punde

Uongozi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Umewapa likizo Wanamichezo wake ili kupunguza mrundikano wa wafanyakazi kikosini humo.

Na.Mwanajuma Juma.Zanzibar
Mwenyekiti wa Idara ya Michezo ya Jeshi hilo Khamis Machenga alisema kuwa hatua hiyo umefanyika kwa lengo la kutekeleza agizo la Serikali la kuondoa mikusanyiko kwa lengo la kujikinga na virusi vya Corona.

Alisema kuwa Jeshi lake linashiriki michezo ya aina mbali mbali ambayo kwa Sasa imesita kutokana na katazo la mikusanyiko hivyo wakaamuwa ni bora kuwapa likizo ili wabaki nyumbani salama.

Machenga alisema kuwa likizo ya wanamichezo hao wapatao karibu 100 ilianza mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kukaa na uongozi wa juu na kikubaliana kufanya hivyo.

"Tumewapa likizo kwa sababu mikusanyiko ipunguwe na hii ni kwa wanamichezo wote waliopo kwenye kikosi chetu", alisema.

Alisema kuwa likizo hiyo imeanza April 17 mwaka huu na watakaa nje mpaka janga hilo litakapomalizika.

Mafunzo inashiriki michezo mbali mbali ikiwemo ya soka, wavu, Kikapu, Netiboli, pamoja na wanamichezo wa Sanaa na Utamaduni kama ngoma za asili, waigizaji na taarabu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.