Habari za Punde

BASHUNGWA AMEWAELEKEZA WAMILIKI WA VIWANDA KUZALISHA VIFAA KINGA VYA KUTOSHA KUKABILIANA NA CORONA.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakiendesha Kikao kilichowakutanisha wamiliki wa viwanda vya vifaa kinga  kwa lengo kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na Corona.  Leo  13.05.2020 jijini Dar es Salaam.
Wadau na wamiliki wa viwanda vya vifaa kinga wakiwa kwenye kikao cha kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na Corona. jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa Pamoja na Waziri wa Afya  Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wameendesha Kikao cha Wadau kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na COVID – 19 leo tarehe 13.05.2020 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua teknolojia na uzalishaji wa  vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.
Kuanzisha viwanda ni sehemu ya ulinzi wa nchi,hivyo kuwa na viwanda vyetu nchini hususani wakati wa shida imesaidia upatikanaji wa baadhi za vifaa kinga kwa bei nafuu.Alisema Waziri Bashungwa
Waziri Bashungwa ameitaka  MSD kununua vifaa kinga vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na vimesajiliwa na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali kununua vifaa hivyo nje ya nchi.
Waziri Bashungwa ameahidi kukitembelea kiwanda cha Msagala Investment kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza kuzalisha malighafi za utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa nchini.
Amesema katika kikao hicho wamekubalia kujipanga vizuri katika uzalishaji wa vifaa kinga na hivyo wamewataka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kujikita katika kuzalisha barakoa aina ya N95 na glove kutokana na kwamba viwanda vya namna hii havipo nchini.
Pia Waziri Bashungwa ameitaka TMDA kushirikia na wizara ya viwanda kuisaidia NDC kuweza  kufanya kiwanda hicho kuanza kuzalisha kwa wakati na hivyo kusaidia watumishi wa afya walio mstari wa mbele kutoa huduma bila hofu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.