Habari za Punde

Diwani wa Wadi ya Magomeni Akusudia Kutowa Huduma ya Kupima Joto la Mwili Wananchi wa Wadi Yake.

Na.Takdir Suweid.
Diwani wa Wadi ya Magomeni Ali Haji Haji amesema anakusudia kuweka utaratibu kupima Joto la mwili Wananchi wake mara kwa mara katika kipindi hiki cha Janga la Covid 19 ili wajuwe Afya zao.
Amesema iwapo Wananchi watatumia kipimo hicho wataweza kujuwa joto la mwili na kujikinga na Virusi vya Corona.
Ameyasema hayo huko Kiwanja cha Mpira kwa Bintihamran wakati alipokuwa akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya kumaliza zoezi la kupima Joto kwa Viongozi wa Wadi hiyo.
Amesema kipimo hicho kitaondosha usumbufu wa Wananchi kukifuata masafa ya mbali na kutumia gharama.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Wadi ya Magomeni Habiba Khamis Ali amesema baadhi ya Wananchi wa Wadi hiyo wanaishi katika maisha magumu na yakubahatisha hivyo wanahitaji kupimwa Joto la Mwili ili kupata  uhakika wa kujuwa afya zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.