Habari za Punde

Mbaroni kwa tuhuma za kumtorosha msichana wa miaka 17

NA MWAJUMA JUMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia Ali Khamis Juma (17), mkaazi wa Chwaka kwa tuhuma za kumtorosha msichana wa miaka 17 jina linahifadhiwa.

Kaimu Kamanda wa Mkoa huo Ramadhan Khamis akizungumzia tukio hilo alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya tukio hilo Mei 24 mwaka huu, huko Chwaka wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema tukio hilo alilitenda  baina ya saa 1:00 na saa 2:00 usiku huko Chwaka kwa kumtorosha msichana bila ya idhini ya wazazi wake na kumpeleka kwenye Banda lake kwa dahimira ya kumuingilia.

Alisema kuwa mshitakiwa huyo yupo chini ya ulinzi na Polisi wanaendelea na uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.