Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Atimiza Ahadi Yake Kwa Wananchi wa Jimbo Lake wa Ubao Waliopata Maafa ya Mvua Kujaa Maji Makaazi Yao.

Mwakilishi wa wananchi jimbo la Tunguu Mheshimiwa Simai Mohammed Said akitimiza ahadi yake ya kuwafariji wananchi kwa kuwasaidia chakula na bidhaa nyengine muhimu kufuatia mafuriko yalioleta athari kubwa katika makazi yao na maeneo ya kilimo katika kijiji cha Ubago, Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati. 
Akikabidhi msaada huo kwa Wananchi wa Kijiji cha Ubago Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kujikimu katika kipindiu hichi cha Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya bidhaa mbalimbali zilizotolewa msaada kwa Wananchi wa Ubago waliopata athari za mvua za masika iliotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja  

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari wakjati wa ziara yake kuwatembelea Wananchi wa jimbo lake waliopata athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Unguja.
Akiwa katika eneo la barabara ya dunga ni moja ya barabara na makaazi ya Wananchi kujaa maji katika kipindi hichi na Wananchi wa eneo hilo kuhama makaazi yao kutokana na kujaa maji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.