Habari za Punde

Serikali yasikitishwa na Tabia za Watendaji wa Taasisi za Ardhi kutokuwa waaminifu


Na.Othman KhamisAme.OMPR.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasikitishwa na tabia ya baadhi ya Watendaji wa Taasisi zinazosimamia masuala ya Ardhi Nchini kuendelea kutokuwa waaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao kitendo ambacho huongeza migogoro ndani ya Jamii Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa masikitiko hayo wakati akijibu Hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kufuatia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake aliyoiwasilisha katika Kikao cha Bajeti cha Baraza hilo kilichoanza siku moja iliyopita.

Balozi Seif Ali Iddi alisema licha ya jitihada kadhaa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali Kuu za kujaribu kupunguza migogoro inayoibuka kila kukicha ya Masuala ya Ardhi lakini bado zipo cheche zinazosababishwa na Watendaji wao vinamatokeo yake walalamikaji kuishia Ofisini kwake kwa kupatiwa ufumbuzi wa kadhia zao.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hivi sasa imekuwa kama jaa la kupokea kero hizo na matokeo yake pale Ofisi inapofuatilia kupata ufumbuzi wa migogoro hiyo Watendaji wake akiwemo yeye binafsi huhusishwa kutumia fursa ya kujimilikisha maeneo ya Ardhi.

“ Mimi sina shida ya Ardhi ya Mtu yeyote nikielewa kwamba hilo ni kosa na dhulma kwa vile tayari nimeshakinai na kuheshimu sheria na taratibu hasa ikizingatiwa kuwa ni Kiongozi Mtendaji Mkuu wa Serikali ninayepaswa kuzisimamia Sheria na taratibu hizo”.

Alitanabahisha Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza Watendaji wanaosimamia masuala ya Ardhi kuwajibika ipasavyo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika misingi ya Sheria ili Haki inayopiganiwa na kila anayedhulumiwa ipatikane.

Akizungumzia safari za nje anazozifanya kwa baadhi ya vipindi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba yapo mafanikio makubwa yanayoibuka ndani ya utaratibu wa safari hizo.

Balozi Seif alisema amekuwa na utaratibu wa safari hizo kuambatana na baadhi ya Mawaziri na Watendaji Waandamizi wa Wizara na Taasisi kutegemea malengo ya safari husika.

Alisema zipo Sekta zilizopata mafanikio makubwa kutokana na safari za nje zinazofanywa na Viongozi Wakuu akitolea mfano Sekta za Elimu, Afya na Kilimo ambazo zimekuwa mihimili ya mazingira bora ya maisha na ustawi wa Wananchi waliowengi hapa Nchini.

Alieleza kwamba fursa za masomo kwa Watendaji na Wanafunzi wa Zanzibar nje ya mataifa yanayofanyiwa ziara na Viongozi hao imekuwa chachu ya Maendeleo yanayoshamiri kila Mwaka.
Akigusiasuala la Dawa za kulevya Nchini ambalo limekuwa sugu na tatizo kubwa Kitaifa na Kimataifa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar janga hili kwa kiasi kikubwa limekuw alikichangia kupunguza nguvu Kazi ya Taifa ambayo ni Vijana wanaotegemewa.

Balozi Seif aliwasihi Wananchi kuachana kwa njia yoyote kushiriki kwenyeu agizaji, uingizaji, usambazaji na hatimae matumizi ya Dawa hizo zenye kuleta athari kuibwa kwa Jamii.
Mapema akitoa ufafanuzi wa kina wa Hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alisema Serikali imefanikiwa kupunguza wimbi la Dawa za kulevya kutokana na jitihada kubwa inayochukuwa ya kupambana dhidi ya wahusika wa tatizo hilo.

Waziri Aboud alisema watu wapatao Mia Tano wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na Dawa za Kulevya, kati ya hao watuhumiwa 503 tayari wameshafikishwa Mahakamani na zaidi ya Kilo 700.73 zimekamatwa kufuatia operesheni maalum za kupambana na Dawa za Kulevya.

Alitahadharisha kwamba wale wote watakaojaribu kuvuruga au kubeza jitihada hizo za mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ambazo zimeshaanza kuonyesha mafanikio, Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria dhidi yao.

Alisema katika jitihada za Serikali za kupambana na Dawa za Kulevya mwaka huu wa Fedha wa 2020/2021 Taasisi inayosimamia Mapambano na Udhibiti wa Dawa za kulevya itatengewa Shingi Bilioni Tatu ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka uliopita ya Shilingi Bilioni Moja.

AlielezakwambafedhahizombaliyakuendeshashughulizaOfisilakinipiazitajumuishanaWatendajiwaTaasisihiyokuendeleakutoaTaalumakwaUmmayajinsiyakupambananaDawazaKulevyakatikamaeneombalimbaliNchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.